Ruka hadi kwenye maudhui makuu

PATRICK PHIRI AINGIWA KIWEWE MECHI YA WATANI

Baada ya kulazimishwa sare ya tatu mfululizo kwenye Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) dhidi ya Stand United juzi, Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia Patrick Phiri amesema "kazi yetu ya ukocha ina majanga, unapokuwa kocha wa soka lazima ukubali kwamba unakaribisha majanga."

Kikianza na washambuliaji wawili wa kimataifa, Mganda Emmanuel Okwi na Mrundi Amissi Tambwe, Kikosi cha Simba kilishikwa kwa sare ya bao moja na Timu ya Stand United kutoka Shinyanga, ikiwa ni sare ya tatu kwa timu hiyo ya Msimbazi katika mechi zake zote za mwanzo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Mara tu baada ya mchezo wa juzi kumalizika katika mahojiano maalum na NIPASHE, Phiri alisema matokeo hayo yamewasikitisha huku akiweka wazi kwamba sare ya tatu imetokana na hofu ambayo wachezaji wake waliipata baada ya wageni Stand United kupata bao la kusawazisha.

"Tuna timu nzuri ingawa makosa madogo madogo yanayofanywa na safu ya ulinzi ndiyo yametugharimu katika mechi zote tatu. Mechi ya leo (juzi) tumecheza vizuri sana kipindi cha pili lakini mambo yaliharibika baada ya wapinzani wetu kupata bao," alisema Phiri na kuongeza:

"Tumekuwa tukitangulia kupata bao katika mechi zote zilizopita lakini tunajikuta tunaambulia sare. Hicho ndicho kilichowapa hofu wachezaji wote baada ya Standd kusawazisha."

Alipoulizwa kuhusu usalama wa ajira yake Simba, Phiri alijibu: "Kazi yetu ya ukocha ina majanga, unapokuwa kocha wa soka lazima ukubali kwamba unakaribisha majanga."
"Ninafanya kazi nzuri kuifundisha Simba lakini makosa madogo madogo yanatugharimu, bahati nzuri soka halichezwi chumbani. Kila mtu anaona namna timu inavyocheza. Sidhani kama mimi ni tatizo Simba.

"Ninaamini nitaendelea kuinoa Simba licha ya matokeo haya. Sare si mbaya kwetu ingawa inauma sana kupata sare katika mazingira haya, tena tunacheza nyumbani," alisema zaidi kocha huyo aliyerejea kwa mara ya tatu nchini kuinoa Simba.

Phiri, aliyewahi kuipa ubingwa Simba bila kupoteza hata mechi moja, rekodi ambayo ilifikiwa na Azam FC msimu uliopita wa VPL, ni kocha wa 18 kuinoa Simba ndani ya miaka 16 tangu 1998, ikiwa ni wastani wa kocha mmoja kila mwaka.

Timu hiyo haina historia nzuri na makocha inayoawaajiri kwani mara nyingi timu inapokuwa na matokeo mabaya, mtu wa kwanza kuwajibishwa huwa ni kocha bila kujali matatizo mengine,

Phiri raia wa Zambia ameanza kuinoa Simba msimu huu baada ya kutimuliwa kwa Mcroatia Zdravko Logarusic Agosti 10 mwaka huu ikiwa ni saa chache baada ya timu kufungwa 3-0 dhidi ya Zesco ya Zambia kwenye Uwanja wa Taifa.

Takwimu za mecghi ya juzi zinaonyesha kuwa Simba ilimiliki mpira kwa kiasi kikubwa kuliko Stand United ikipata kona tisa dhidi ya nne za wageni, mashuti 10 dhidi ya manne ya Stand United, kuotea mara mbili dhidi ya moja ya wageni na kufanya rafu mara 13 dhidi ya 17 za wageni.

Tambwe na Ramadhani Singano 'Messi' ndiyo waliootea upande wa Simba huku Jonas Mkude akiwa ni mchezaji pekee wa Simba aliyeonyeshwa kadi ya njano. 

Kocha wa Stand United, Emmanuel Masawe alisema sare mbili za mwanzo ambazo Simba ilitoka 2-2 dhidi ya Coastal Union na 1-1 dhidi ya Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Taifa, ndiyo zilizoiua timu hiyo katika mechi ya juzi.

"Matokeo ya awali ndiyo yamewaua Simba katika mechi yetu ya leo (juzi). Wanacheza kwa presha kubwa ya mashabiki wao ambao wanaonekana kukatishwa tamaa na timu yao. Hicho ndicho kimewagharimu," alisema kaka huyo wa mchezaji bora wa VPL msimu wa 2011/12, Jacob Masawe.

Takwimu Kona Rafu Mashuti Kuotea Njano Simba 9    13    10     2    1
Stand United                                                                    4      17    4      1    3

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC