Ruka hadi kwenye maudhui makuu

NYERERE DAY: TUMUENZI NYERERE KWA VITENDO



Ili kumuenzi Nyerere, TFF irejeshe kombe lake

Na Fikiri Salum

WATANZANIA wameadhimisha siku ya kumbukumbu ya kifo chake rais wa kwanza wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Julius Kambarage Nyerere ambaye alifariki Oktoba 14 mwaka 1999 katika hospitali ya Mtakatifu Thomas nchini Uingereza.

Ni miaka 15 tangia kifo chake ambapo kuna mengi ya kukumbuka enzi za utawala wake, kumbukumbu ya Nyerere ndiyo imenisukuma hadi kuandika makala hii, Watanzania wengi wamekuwa wakimzungumzia Mwalimu kutokana nay ale aliyofanya ambapo wengi wao wanasema bado Watanzania wameshindwa kumuenzi kwa vitendo.


Inawezekana ni kweli Watanzania wameshindwa kumuenzi kwa vitendo mwalimu Nyerere na hutumia magazeti na vyombo vingine vya habari kumuenzi huku vitendo hakuna, rushwa imechukua nafasi ambapo sasa hivi imeonekana kama fasheni, ukienda hospitali lazima utumie rushwa ili uhudumiwe haraka.
Ipo hivyo hata polisi, lazima rushwa itumike ili kumtoa ndugu yako aliyeshikiliwa au wewe mwenyewe, kama hivyo basi ataendelea kusota rumande, mahakamani ambapo ndiko kunakoaminika kwa sheria lakini siku hizi nako kumebadilika, ili kesi iende haraka itakugharimu utoe kitu kidogo.

Kusema kweli mambo siku hizi hayaendi ipasavyo na rushwa imekuwa kama haki vile, katika makala yangu ya leo namzungumzia mwalimu Nyerere ambaye muasisi wa taifa hili, Nyerere ni mmoja kati ya wanaharakati wa kwanza nchini waliopigania uhuru wan chi hii.

Kutokuwepo kwake kumefanya jitihada kadhaa alizokuwa anazipigania kukwama, Nyerere alipenda watu wake wawe na uhuru wa kweli baada ya kuupata kutoka kwenye minyororo ya Wakoloni, Tanganyika baadaye Tanzania ilitawaliwa na Wajerumani na baadaye Waingereza.

Nyerere alitumia mchezo wa soka ili kupigania uhuru wan chi hii, pia alifanikisha muungano kati yetu na Zanzibar ambayo nayo ilikuwa katika utawala wa kimabavu wa Sultan wa Oman na Waingereza, baada ya kuungana na kuwa taifa moja Tanzania, Nyerere aliendelea kusaidia juhudi mbalimbali katika michezo.
Enzi zake alihakikisha timu za taifa zinafanya vizuri na kuwakilisha vema Tanzania na kweli ili9kuwa hivyo ambapo timu ya taifa ya riadha ilifanya kweli katika mashindano ya Madola yaliyofanyika Scotland ambapo mwanariadha Filbert Bayi alivunja rekodi ya dunia.

Haikuwa kwa Bayi peke yake isipokuwa wanariadha wengine kama Seleman Nyambui, Juma Ikhangaa na wengineo walifanya kweli, Tanzania ilisifika katika mchezo wa riadha kiasi kwamba majirani zetu Kenya walisubiri kwanza, lakini sasa hivi Kenya iko mbele na Tanzania inasuasua.

Nyerere tutamkumbuka kwa mengi hasa pale alipoteua waziri wa elimu na utamaduni ambaye alipigana kwa nguvu zote kuhakikisha Tanzania inafanya kweli katika michezo, michezo ilishamili hadi mashuleni ambapo masomo maalum ya michezo yalienziwa.

Katika harakati zake za kisiasa Nyerere hukuwa nyuma katika kupenda michezo hasa soka, TFF inapaswa kumuenzi

Mbali na michezo mashuleni kuenziwa, timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania ilikuwa miongoni mwa timu tishio barani Afrika, mwaka 1980, Taifa Stars ilifuzu fainali za mataifa huru barani Afrika (Mataifa Afrika) iliyokuwa inafanyika nchini Nigeria.

Stars ilikwenda kushiriki fainali hizo zilizokuwa zinashirikisha timu za mataifa manane tu tofauti na sasa mataifa 16 yanashiriki, hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza Taifa Stars kushiriki fainali hizo na pia ni mara ya mwisho, hadi sasa Stars haijashiriki fainali hizo zaidi zaidi ilishiriki fainali za mataifa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani CHAN.

Nyerere tutaendelea kumkumbuka kutokana na juhudi zake binafsi ambapo alianzisha vyama mbalimbali vya kusimamia michezo hapa nchini, TFF zamani FAT iliasisiwa enzi za Nyerere hivyo ni moja kati ya zao lake, katika taasisi hiyo kubwa nchini imeshindwa kumuenzi barabara.

TFF imeshindwa kuyarejesha mashindano yalikuwepo zamani ya kombe la Nyerere ambayo yalikuwana hadhi kubwa, mashindano hayo ya mpira wa miguu yalishirikisha timu zinazoshiriki ligi kuunamadaraja mengine ambapo bingwa anapata tiketi ya kushiriki kombe la CAF sasa Shirikisho.

Nakumbuka michuano hiyo ilifanyika mara mbili ambapo timu ya JKT Ruvu ya Pwani ndio ilikuwa mabingwa na ilipata nafasi ya kushiriki kombe la Washindi barani Afrika lakini TFF wakati FAT ilishindwa kuwasilisha majina ya wachezaji wake CAF na kufanya iondolewe katika michuano hiyo.

Baadaye Tanzania ilisimamishwa na CAF kutokana na kutopeleka wawakilishi katika michuano ya CAF, uzembe huo ulifanyika na baadaye kombe la Nyerere likashindwa kufanyika, kushindwa kufanyika kwa kombe la Nyerere kulitokana na uzembe wa viongozi wa FAT.

Wakati sasa TFF inaongozwa na Jamal Malinzi ambaye wakati akinadi kampeni zake za kuingia madarakani aliahidi kuyarejesha mashindano hayo ya mwalimu Nyerere, Malinzi amefikisha mwaka mmoja tangia aingie TFF lakini bado hajaweza kutimiza ahadi yake.

Baba wa Taifa Mwl Julius K Nyerere ni mmoja kati ya wapenda michezo ambaye anapaswa kuenziwa

Ili kumuenzi Nyerere michuano yake yenye jina lake inapaswa kurejeshwa ili kuenzi mema yake na mchango wake mkubwa alioutoa kwenye soka, Kama Watanzania wanaamini kuwepo kwa viongozi wa dini siku timu ya taifa, Taifa Stars inawafunga Benin pale kwenye uwanja wa Taifa mabao 4-1 basi uwepo wa michuano ya Nyerere Cup kunaweza kuleta Baraka nyingine na kubwa kwenye soka la nchi hii.

Jina la Nyerere limetapakaa kila mahari lakini  michuano ya Nyerere Cup ndiyo pekee inaweza kulienzi jina hilo, pia michuano ya Nyerere inazishirikisha timu kubwa na kongwe hapa nchini kama Yanga na Simba hivyo inaweza kutumika kupatikana kwa fedha ambazo zinaweza kuingia katika mfuko wake wa Nyerere Foundation.

Bado mwalimu Nyerere ni muhimu katika maendeleo ya soka letu kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa, Nyerere alihakikisha klabu kongwe za Simba na Yanga zinadumu katika soka la nchi hii, timu hizo zilitumika kuunganisha umoja ambapo ndio sera kubwa ya mwalimu.

Simba na Yanga zilitumika kuhakikisha amani ya nchi hii inaendelea kwani timu hizo zimekuwa na mashabiki wengi na nusu yake ni sawa na theluthi mbili ya Watanzania wote, kuwepo kwa Simba na Yanga kumechangia kuwepo kwa mshikamano baina ya Watanzania na majirani zao, timu hizo zimekuwa zikishiriki mara kwa mara michuano ya klabu bingwa Afrikamashariki na kati.

Namkumbusha tena rais wa TFF Jamal  Malinzi kuyarejesha mashindano ya kombe la Nyerere ili kumuenzi muasisi huyo wa taifa hili, Mwenyezi mungu amuweke mahara pema peponi Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Burito Wanzagi Nyerere, 0755 522216.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC