Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAKALA: SIMBA NA YANGA NI MABOMU YANAYOSUBIRI ZAMU YA KULIPUKA


Na Prince Hoza



NINGEANZA kwa pongezi kwa timu ya taifa, Taifa Stars ambapo mwshoni mwa wiki ilifanikiwa kuilaza timu ngumu ya taifa ya Benin katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotambuliwa na shirikisho la soka duniani Fifa, mchezo huo ulifanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kufanyika mchezo huo kulitanguliwa na mchezo wa kirafiki kati ya waumini wa dini mbili za Kiislamu na Kikristo, katika mchezo huo waumini hao walijigawanya katika timu mbili na moja iliitwa Amani na nyingine iliitwa Mshikamano, Aman ilishinda 1-0 goli likifungwa na Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.


Vile vile klabu ya Simba bado iko nchini Afrika Kusini ikijiandaa na mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya hasimu wake mkuu Yanga, Simba imeamua kuweka kambi nchini humo na kucheza mechi mbili za kajaribio.

Timu hizo zote zinaingia uwanjani zikiwa tayari zimeshacheza mechi tatu kila mmoja, Simba ilianza ligi kwa kucheza na Coastal Union ya Tanga katika uwanja wa Taifa ambapo matokeo yalikuwa sare ya kufungana 2-2, aidha ilishuka tena katika uwanja huo huo wa Taifa na kucheza na Polisi Moro ambapo matokeo yaliendelea kuwa sare ya 1-1.

Matokeo hayo yaliwaudhi mashabiki wake hasa kutokana na usajili wa msimu huu Simba imeonekana kuimarika, Simba iliwasajili nyota Emmanuel Okwi, Pierre Kwizera, Manyika Peter, Hussein Sharrif ‘Casilass’, Paul Kiongera, Ibrahim Hajibu, Joram Mgeveke na wengineo.

Pia iliimarisha benchi la ufundi kwa kumrejesha aliyekuwa kocha wake mwewnye mafanikio na timu hiyo Mzambia Patrick Phiri, awali Simba ilikuwa ikinolewa na Mcrotia Zdravko Logarusic, kuajiliwa kwa Phiri na kusajiliwa kwa Okwi na Kiongera kumewafanya mashabiki wa Simba kutembea vifua mbele.

Okwi anafahamika kwa kiwango chake cha juu na Kiongera alianza kuwaonyesha mavitu mashabiki wa Simba katika mecho za kirafiki, mchezaji huyo raia wa Kenya alionyesha uwezo mkubwa wa kuuchezea mpira na kuwapa matumaini mashabiki wa  timu hiyo.

Hata hivyo Simba imeanza ligi vibaya kwa kutoka sare mechi tatu mfululizo, Simba ilikuwa kambini visiwani Zanzibar ambapo ilicheza mechi kadhaa za kirafiki kabla haijarejea kuanza ligi, mchezo wa tatu wa Simba ilicheza na Stand United ya Shinyanga katika uwanja wa Taifa ambapo matokeo yalikuwa 1-1.

Kutokana na mwenendo huo mbaya was are ilioanza nao Simba imeamua kuondoka nchini na kukimbilia Afrika Kusini huenda mambo yakabadilika, pia tayari minong’ono ya chini kwa chini imeanza katika klabu ya Simba ambapo kuna watu wanahusishwa na matokeo hayo, inasemekana kundi la wanachama waliosimamishwa maarufu kama Ukawa ndio wanaotupiwa macho.

Marcio Maximo akiwa na straika anayemuamini Jaja, lakini Yanga ikifungwa na Simba ujue lawama inamndokea yeye kwa kumbeba Mbrazil mwenzake

Ingawa hakuna ushahidi wowote kama wanahu7sika moja kwa moja lakini wanachama hao nano wamekuwa na ishara zao zinazoashiria kuna mgogoro unafukuta ndani ya Simba, lakini kuna malalamiko mengine kuwa uongozi wa sasa wa Simba chini ya rais Evans Aveva umewabagua wazee wa klabu hiyo wakiongonzwa na mzee Hamisi Kilomoni.

Kuwatimua wazee hao kumepelekea baadhi ya mambo kuyumba, hivyo kuna uwezekano mkubwa Simba ikaanza ligi na mtani wake kwa furaha ama kupoteza au kuendelea na sare zake kama kawaida, Kwa upande wa Yanga nako ni hivyo hivyo kama Simba ingawa kuna tofauti kidogo.
Kikosi cha Yanga kiliweka kambi yake Visiwani Pemba, ilicheza mechi kadhaa za kirafiki kabla ya haijaingia katika mechi za ligi, Yanga nayo imefanya usajili wake makini msimu huu kwa kuwasajili Wabrazil Andrey Coutinho na Geilson Santana Santos Jaja, pia iliimarisha benchi lake la ufundi baada ya kuondokewa na mwalimu wake Mholanzi Hans Van Der Pluijm na msaidizi wake Charles Boniface Mkwassa.
Yanga iliamua kumchukua aliyekuwa kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars Mbrazil Marcio Maximo, pia ikamchukua msaidizi wa Maximo ambaye naye ni Mbrazil Leonaldo Neiva, Yanga iliendelea kuimarisha benchi lake la ufundi kwa kuwaajili wachezaji wake wa zamani Shadrack Nsajigwa na Salvatory Edward kuwa makocha wasaidizi.

Yanga ilianza ligi vibaya kwa kupoteza dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo uliofanyika mjini Morogoro kwenye uwanja wa Jamhuri, pia ikafufua matumaini yake kwa kuzilaza Prisons ya Mbeya na JKT Ruvu ya Pwani mabao 2-1 , Yanga imefikisha pointi sita huku mtani wake Simba akiwa na pointi 3.

Karibu vikosi vya timu zote vipo imara na kila mmoja anatambia kikosi chake hivyo tarehe 18 ndiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa, lakini vilabu hivi kila vinapokutana vimekuwa na kila aina ya tambo na mmoja wapo anapopoteza mchezo huanza kunagusha lawama kwa benchi lake la ufundi au wachezaji.
Utasikia mchezaji Fulani amehujumu, au kocha awezi kazi ameshindwa kuendana na timu yetu, tayari timu hizo zimefukuza makocha wengi katika kipindi cha miaka miwil, Yanga tangia 2009-2014 imeshatimua makocha zaidi sita wakati mtani wake Simba naye ni hivyo hivyo.

Timu timua yao inatokana na mchezo wa Simba na Yanga au kuvurunda katika mechi kadhaa na kuinyima timu ubingwa, siwezi kushangaa kusikia Yanga imemtimua kocha wake baada ya kufungwa na Simba, au Simba imemtimua kocha wake baada ya kufungwa na Yanga.

Simba ikishinda ataonekana bonge la kocha, lakini ikifungwa atadhauliuliwa na kufukuzwa

Sitashangaa kusikia mchezaji Fulani kasimamishwa na Yanga kufuatia matokeo mabovu dhidi ya Simba au Simba imemtimua mchezaji wake Fulani kufuatia matokeo mabovu dhidi ya Yanga, timu hizi ni kama bomu linalosubiri kulipuka. 

Vuguvugu la chini kwa chini lililopo Simba mwisho wake litamalizika kwa mpambano huu wa watani endapo Simba itashinda utasikia sasa hakuna vurugu za chini chini kwa wanachama wote wa Simba ni kitu kimoja, hata wale wazee waliochukizwa baada ya kutimuliwa na uongozi mpya nao pia shwari.

Lakini kinyume na hapo utasikia balaa lake, kwa upande wa Yanga kule kuko kimya muda mrefu hasa baada ya wale wanachama waliokuwa wanampinga mwenyekiti wao Yusuf Manji kwa kuj9ongezea mudea nao utawasikia endapo Yanga imepoteza, watakuja na hoja yao ya kumng’oa kabisa kuwa Manji hawafai Wanayanga na anaidhalilisha Yanga, Kikubwa wanachama hao watapata nguvu kutoka kwa wanachama wengine waliochukizwa na kipigo toka kwa Simba, hapo ndipo bomu linapolipuka.

Kitu kikubwa na cha muhimu ni kusubiri kisha tuone, sina mengi sana wadau wangu isipokuwa tuombe mungu siku ya siku ifike tushuhudie mpambano wa kihistoria, timu hizi msimu uliopita hazikufungana kabisa, mechi zote mbili zilitoka sare, walianza katika mzunguko wa kwanza ambapo walifungana 3-3 na mzunguko wa pili 1-1, 0652 626627

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC