Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAKALA: KINACHOTOKEA SIMBA SASA NI UHARIFU KWA WACHEZAJI, HANSPOPPE AOMBE RADHI, SPUTANZA NI WAKATI WENU SASA KUKEMEAS



AWALI wakati wa majira ya usajili nchini, timu ya kandanda ya Simba SC iliamua kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake.

Ikiwa chini ya rais, Evance Aveva, Simba iliamua kumfuta kazi aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Mcroatia, Zdravko Logarusic na kumuajiri, Patrick Phiri kutoka Zambia.

Mabadiliko yalifanyika hasa, wachezaji wa kila aina walisajiliwa huku wale walioshindwa kufanya vizuri msimu uliopita wakiachwa.

Lengo ya uongozi mpya ilikuwa ni kuifanya klabu ya Simba kurudi katika hali yake ya ushindani ambayo katika kipindi cha miezi 34 sasa imeshuka kwa kiwango kikubwa.


Sijui sana kuhusu mwanzo wa tawala nyingine katika timu hiyo ulivyokuwa, lakini katika kipindi cha siku 14 za karibuni nadiriki kusema, uongozi wa sasa umeanza vibaya zaidi. Sababu ni nyingi lakini kubwa zaidi ipo katika utawala.

Simba inayumbishwa na viongozi wake wenyewe ambao wanakataa kukubali makosa waliyofanya mara baada ya kuingia madarakani.

Kitendo cha kuwafuta uanachama baadhi ya waliokuwa wanachama wa klabu hiyo kinawagharimu wakati huu. Ulikuwa ni uamuzi ‘ mbaya’ ambao awali nilisema utakuwa tatizo kwa timu.

Hapa sizungumzii kuhusu sera za Aveva ambazo zilimfanya aingie madarakani, kwani kama utazama na kugusa huko vile ilivyo sasa ‘ ameshindwa vibaya’, alikuwa na sera mbovu, lakini si hivyo ‘ sera ya pointi 3’ imekufa, hivyo ni lazima zitazamwe sababu zilizofanya sera hiyo kutokuwa na mafanikio.

Katika mchezo wa kwanza wa msimu huu, Simba ilicheza na Coastal Union ya Tanga katika uwanja wa Taifa, ilionekana kama vile mambo yatakwenda sawa msimu huu baada ya Shaaban Kisiga kufunga bao la ‘ mkwaju wa penalti’.

Lilikuwa bao la kwanza la msimu kwa Simba, na lilifungwa na mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kikosini tena ‘ kwa kutumia maarifa binafsi’.

Amis Tambwe akafunga bao la pili, lakini mambo yalikuwa magumu dakika 25 za mwisho. Coastal walichomoa mabao yote na kutengeneza sare ya kufungana mabao 2-2. Halikuwa tatizo, hakukuwa na hujuma.

Hanspoppe: Mzee mzima umechemsha kabisa kutokana na kauli zako zisizo za kitaalamu kuhusu Kiemba, Chanongo na Kisiga wakati jamaa wanajituma sana

Mchezo wa pili ulikuwa ni dhidi ya Polisi Morogoro, pia ulipigwa katika uwanja wa Taifa. Simba iliongoza kwa bao la mshambulizi, Emmanuel Okwi.

Ndani ya nusu saa ya mchezo. Mshambulizi wa zamani wa Simba Danny Mrwanda akiitumia vizuri ‘ pasi ya kupenya’ iliyopigwa na kiungo Salum Machaku na kuisawzishia timu yake dakika tano tu mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili.

Mechi ikamalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1. Hapa kidogo maswali yakaanza kujitokeza, kiwango kibovu kutoka kwa baadhi ya wachezaji kilifanya wengi kuanza kujiuliza kulikoni.

Katika hali ya kutojiamini, ama kutoheshimu timu pinzani. Uongozi wa Simba ulikaa chini na kufikia mwafaka wa kuhitisha kikao cha siri kati ya utawala, benchi la ufundi na wachezaji.

Bila uoga baadhi ya wachezaji walisema kuwa matokeo ya sare mbili mfululizo yaliletwa na ushirikiano mdogo uliopo katika timu.

Hawakugusia mambo yaliyopo katika uongozi bali walisema ‘ wachezaji kwa wachezaji’ hawapeani ushirikiano ule wa kimpira wakiwa uwanjani.

Ilikuwa ni hoja ambayo ndani yake ina mantiki kwa sababu kuna baadhi ya viongozi wameonekana kuwagawa baadhi ya wachezaji na kuwapendelea wengine kwa sababu tu mchezaji Fulani hajasajiliwa na ‘mtu/watu fulani’.

Baada ya kikao hicho mambo yalikwenda vilevile. Mchezo wa tatu ulikuwa ni dhidi ya Stand United ya Shinyanga ambao nao ulifanyika katika uwanja wa Taifa.

Kisiga akitokea benchi kuchukua nafasi ya Said Ndemla aliyeumia alifunga bao lake la pili msimu huu, pia lilikuwa bao la mkwaju ‘ uliokufa’.

Katika ligi ambayo mabao kadhaa yamefungwa kwa mipira ya adhabu ndogo, Kisiga anaweza kuipa Simba pointi ‘ tatu za kwanza’ msimu huu kama tu safu ya ulinzi isingeendeleza ‘ tabia yao ya kukubali kuruhusu bao la kuswazishwa’.

Mwishoni mwa mchezo Stand walichomoa na kutengeneza sare ya Tatu mfululizo katika uwanja wa nyumbani’.

Phiri: Amekalia kuti kavu muda wowote anaweza kutupiwa virago kufuatia sare kuiandama Simba

Katika mchezo wowote huwa tunasema; ‘ asiyekubali kushindwa, si mshindani’, lakini katika fikra za kishabiki, matokeo ya Simba yalipangwa.

Hivyo ndivyo wanavyoamini baadhi ya viongozi. Nahodha, Joseph Owino aliwekwa benchi katika mchezo dhidi ya Stand na nafasi yake kuchezwa na chipukizi, Joram Mvegeke.

Sijui kama yalikuwa ni mapendekezo ya Phiri mwenyewe kama mkuu wa benchi la ufundi, au ni muendelezo wa makocha ‘ dhaifu wa kigeni’ ambao wanaendeshwa ‘ kwa rimoti’ na baadhi ya watu wenye kuwashikilia?.

Kama tatizo la kwanza ilionekana ni Owino, Simba hawakung’amua chanzo cha tatizo lenyewe.

Je, baada ya Owino kuwekwa benchi, safu ya ulinzi ilifanya kazi nzuri zaidi?. Matokeo yalikuwa ni ‘ yale yale tu’. Mchezaji pekee ambaye hajakosekana katika safu ya ulinzi ya Simba msimu huu ni Hassan Isihaka.

Kiwango chake ni kizuri lakini kama sababu ni hujuma, wengine wote waliofanyiwa mabadiliko hawakuleta afadhali yoyote hadi pale Owino alirudishwa katika mchezo dhidi ya Yanga ambao ni pekee Simba hawakufunga bao wala kuruhusu goli msimu huu.

Kisiga: Ndio mfungaji pekee wa Simba msimu huu aliyeifanya iamke licha ya sare tano mfululizo

Kihistoria, Simba ilipaswa kuchukua pointi tatu dhidi ya Polisi Moro kwa sababu huwa hawana uwezo wa kuifunga timu hiyo ya Morogoro ikiwa nyumbani katika miaka ya karibuni.

Sare dhidi ya Coastal ni kielelezo cha ugumu wa ligi ya msimu huu, sare ya Stand ni matokeo ya soka tu. Huku suluhu dhidi ya Yanga ilichukuliwa kama ‘ mwisho wa matatizo’. Hawakujua, kumbe ni mwanzo wa kuelekea kipigo cha kwanza msimu huu.

Wakati Fulani msimu uliopita ulipokuwa ukielekea mwishoni, niliwahi kuhoji kiwango cha kiungo Haroun Chanongo. Ukweli wakati ule wa mchezo dhidi ya Mbeya City uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 niliamini kuwa, Chanongo ni mchezaji mwenye ‘ tabia ya kupanda na kushuka kwa kiwango chake’.

Lakini kuanzia msimu huu, mchezaji huyo amekuwa juu, lakini ametimuliwa kambini kwa sababu za kudaiwa kuchangia matokeo mabaya ya timu. Kivipi?

Okwi alifunga bao la kuongoza kwa timu yake na kuifanya iwe mbele kwa bao 1-0 katika uwanja ambao wameishinda, Tanzania Prisons mara mbili tu katika kipindi cha miaka 14 sasa.

Zikiwa zimesalia dakika tano mchezo kumalizika Prisons waliswazisha. Simba imepata pointi ya kwanza katika uwanja wa ugenini msimu huu baada ya kufungana bao 1-1 na Prisons lakini hilo limeambatana na kusimamishwa kwa baadhi ya wachezaji.

Chanongo, Kiemba na Kisiga. Lakini katika hali ya kimpira tuhuma hizo si za kweli zaidi ya ‘ chuki binafsi alizonazo’ mwenyekiti wa kamati ya usajili kwa wachezaji hao ambao hakuwasajili yeye.

Haruna Chanongo msimu huu amerejea katika kiwango chake tofauti na viongozi wanavyodai hadi kumsimamisha

Majuzi alisikia mwenyekiti huyo wa kamati ya usajili akisema kuwa kila anapopangwa Kiemba timu yao haishindi. Je, huu ndiyo weledi wa kiuongozi. Ule mgawanyiko ambao wachezaji waliusema katika kikao unaletwa na viongozi kama hawa ambao wanasema tu wachojisikia.

Nathubutu kusema kuwa baada ya sare tano mfululizo, Simba itapigwa na Mtibwa Sugar wikiendi ijayo na baada ya hapo atakayefuata ni kocha Patrick Phiri.

Lakini Simba SC inaharibiwa na hao jamaa zao wenyewe, ‘ Watu wakubwa’. Wakati wa uongozi wa Mh. Aden Rage nilikuwa nikipenda kutumia sentesi ya ‘ Mtu mkubwa ni Mwanafunzi’, hutamani vitu vingi zaidi.

Labda Phiri apange wachezaji wote waliosajiliwa na ‘ Mbwana Mkubwa’ ndipo Simba itashinda!!. Nyakati za furaha zimepotea klabuni huku ndani ya uwanja matokeo yakiwa ‘ hovyo’.

Msiwape lawama ‘ wale-Simba Ukawa’ ambao hawajulikani wanaishi wapi, ‘ adui wa kwanza wa Simba ni Pesa’, Si Kiemba, Kisiga wala Chanongo. Niliwahi kuandika ‘ Phiri atafukuzwa kazi Simba SC….

Phiri yupo katika ‘ shinikizo la chinichini’ hivi sasa. Hakuna, Simba ukawa ila kuna watu ndani ya Simba yenyewe wanataka Simba ifungwe sasa na si kutoa sare, unajua ni kwa nini? Mtu mkubwa ni Mwanafunzi tu.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC