Ruka hadi kwenye maudhui makuu

WEMA SEPETU ATOSWA JUMLA NA DIAMOND, SASA MENINAH KUOLEWA

Habari mpya zinasema kuwa vikao vya harusi ya Diamond na Meninah ambaye ni mwanamuziki wa Bongo fleva vimeanza kimya kimya nyumbani kwa mama Diamond huku mmoja wa wahudhuriaji wakiwa ni mama Diamond mwenyewe na Queen Darlin ambaye ni dada wa Diamond.

Kwa mujibu wa Baabkubwa magazine  paparazzi wake alienda nyumbani kwa Diamond hivi juzi kati kufanya nae mahojiano hata hivyo hakumkuta Diamond lakini alimkuta mmoja wa watu wake wa karibu ambaye yupo pia upande wa Wema Sepetu.

Chanzo hicho kilimwaga news kuwa hakuna cha ndoa ya Diamond na Wema bali ndoa inayopangwa kwasasa ni ya Diamond na Meninah na vikao vimeanza kwa mama Diamond.

Chanzo hicho kilisema kuwa Diamond na Meninah walikutana takribani miezi mitano iliyopita wakati wa maandalizi ya tuzo za Kili Awards 2014 ambapo wote walitumbuiza.


Baada ya hapo wakaingia mapenzini kimya kimya mpaka wiki za hivi karibuni gazeti moja lilipovujisha habari hizo za mahaba ya Diamond na Meninah na media nyinmgine kuziandika kwa kasi.

Kwa mujibu wa chanzo hicho ni kuwa Wema ametoswa sababu ya kuendekeza pombe inayompelekea kuwa mvivu na kutotaka kufanya kazi badala yake ni starehe tupu, kwa maana kuwa hata nyumbani kwa mama Diamond haendi mara kwa mara kumsalimia inaweza hata kupita miezi 3 hajaenda ila Meninah anaenda na akifika kule humsaidia mama Diamond kazi, kupika na kupakua.

Chanzo hicho kimesema kuwa hata Wema anajua kuwa Diamond na Meninah wana ishara zote za kuwa wapenzi lakini hana cha kufanya, huku Meninah yeye akiwa tayari amejitoa muhanga kwa Diamond lakini anawaogopa Team Wema kumshambulia hasa kwa mvua za matusi kama ilivyo kawaida yao lakini mama Diamond anampoza kuwa asiwe na shaka yeye kamkubali Diamond hawezi kukataa kumuoa hilo amuachie yeye mama Diamond.

Vikao hivyo licha ya kuhudhuriwa na mama Diamond na Queen Darleen, chanzo hicho kimesema pia kuwa kuna ndugu wengine wa Diamond na mama Diamond wanahudhuria ila yeye hawajui sababu hana ukaribu nao.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC