Ruka hadi kwenye maudhui makuu

PHIRI AMKUBALI JAJA, AWATAKA SIMBA KUJIPANGA

Kocha wa Simba, Patrick Phiri amesema nyota wa Yanga, Genilson Santos ‘Jaja’ ni mshambuliaji hatari na mwenye akili nyingi anapofika golini.

Phiri alimshuhudia Jaja akifunga mabao mawili na kuiongoza Yanga kushinda 3-0 dhidi ya Azam katika mchezo wa Ngao ya Jamii.

Mzambia huyo, Phiri, alilimbia gazeti hili kuwa licha ya watu wengi kumbeza Jaja, lakini ni mshambuliaji hatari anapolikaribia lango na hapaswi kukabwa na mabeki legelege kwani wakati wowote anaweza kufunga.


Phiri alisema Jaja ana nguvu licha ya kutokuwa na kasi,  lakini ana uamuzi mzuri anapokuwa karibu na lango, kitu ambacho washambuliaji wengi hawana. 

“Ni mchezaji mzuri, nimependa anavyofanya uamuzi  anapofika katika eneo la hatari, ana uamuzi wa haraka ambao wengi hawategemei, licha ya kuwa ni mzito, lakini ni hatari na anapaswa kuchungwa mno na mabeki.

Kikosi cha Phiri kitaivaa Yanga Oktoba 12, hivyo amewataka mabeki wake kuwa makini watakapocheza na Yanga, ambao safu yao ya ushambuliaji sasa itakuwa ikiongozwa na Jaja.

“Tunatakiwa kumuangalia sana siku tutakapokutana na Yanga, inabidi tumfungie kazi, nimependa jinsi alivyofunga lile bao la pili, washambuliaji wengi wasingeweza kufanya kile alichokifanya, anaonyesha ana akili,” alisema Phiri.

Jaja alipata wakati mgumu katika mchezo huo ulipoanza kiasi cha kufikia baadhi ya mashabiki wa Yanga kumpa presha kocha Marcio Maximo amtoe, lakini kocha huyo Mbrazil ni kama aliweka pamba masikioni huku akiamini  mchezaji huyo atawanyamazisha.

Katika hatua nyingine, Maximo alisema alilazimika kutumia mifumo mitatu tofauti katika mchezo wao dhidi ya Azam.

“Nilianza na mfumo wa kukaba eneo la katikati nikimtumia Said Juma aliyemudu vema nafasi hiyo na baadae kumtoa na kumuingiza Hassan Dilunga naye alifanya kazi niliyomtuma ipasavyo,” alisema Maximo.

Kocha huyo aliongeza kuwa baada ya kuona wapinzani wao wamepoteana katikati ya uwanja aliwataka wachezaji wake kupiga mipira mirefu kwa kutumia kasi ya Mrisho Ngasa na Simon Msuva.

“Niliamua kumtoa Nizar (Khalfani) na kumuingiza Msuva, ambaye ana kasi na aliimudu nafasi yake pia kama ilivyokuwa kwa wengine walioingia,” alisema kocha huyo na kuongeza

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Ngao ya Jamii sasa ni Simba na Yanga

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limebadilisha kanuni za mashindano za Ngao ya Jamii kutoka timu nne na sasa utaratibu utakuwa kama zamani. Bingwa wa Ligi Kuu bara atacheza na mshindi wa kombe la CRDB Cup "CRDB Federation Cup, na endapo kama bingwa wa ligi na CRDB atakuwa ni mmoja basi mshindi wa pili kwenye Ligi Kuu ya NBC atacheza mchezo wa ufunguzi wa ligi yaani Ngao ya Jamii.  Hivyo ni rasmi ufunguzi wa wa ligi kuu mchezo  wa "Ngao ya Jamii msimu huu 2025-2026 ni Yanga na Simba watakutana.

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...