Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MESSI ATIKISA, SUAREZ AANZA KAZI BARCELONA IKIUA 6-0

Luis Suarez

Luis Suarez alichezea Barcelona mechi yake ya kwanza baada ya kuhamia huko kutoka Liverpool kwa €95 milioni huku klabu hiyo ya Catalona ikikomoa Club Leon ya Mexico 6-0 mechi ya kirafiki Jumatatu.

Straika huyo wa Uruguay, ambaye hataweza kuchezea Barca mechi ya ushindani hadi Oktoba baada ya rufaa yake dhidi ya marufuku ya miezi minne kutokana na kumng’ata difenda wa Italia Giorgio Chiellini wakati wa Kombe la Dunia kukataliwa wiki iliyopita, alitolewa na nafasi yake kujazwa na Rafinha Alcantara dakika 14 kabla ya mechi kumalizika.

Barca walikuwa tayari wanaongoza 4-0 kutokana na mabao ya Lionel Messi, Munir El Haddadi na mawili kutoka kwa Neymar kabla ya Munir na Sandro kukamilisha ufungaji mabao yao.


Licha ya utata unaozingira historia yake, ambao ni pamoja na marufuku mara mbili awali kwa kuuma wachezaji pamoja na kusimamishwa kucheza na Shirikisho la Soka la Uingereza kwa kumtusi kwa ubaguzi wa rangi difenda wa Manchester United Patrice Evra, Suarez alikaribishwa vyema na mashabiki wa nyumbani alipoingia uwanjani.

Awali, Neymar na Messi walicheza vyema sana mechi yao ya kwanza tangu ndoto yao ya Kombe la Dunia kuisha vibaya kwa jeraha mbaya la mgongo na kichapo fainali mtawalia.
Messi alifunga la kwanza kwa kichwa dakika tatu kutoka kwa krosi ya Neymar iliyokuwa imepinduliwa.
Straika huyo wa Brazil baadaye aliongeza la pili kwa ustadi baada ya kupokea mpira kutoka kwa Andres Iniesta kabla ya kujifungia lake la pili usiku huo kwa kisigino kwenye wavu wazi dakika mbili kabla ya muda wa mapumziko.

Munir aliingia badala ya Neymar wakati wa mapumziko na akafunga la nne pale Dani Alves alipogonga mpira kutoka kwa Ivan Rakitic na ukaanguka katika njia ya mchezaji huyo wa miaka 19.
Na muda mfupi baada ya Suarez kuingia, Munir alifunga lake la pili kwa kombora zito la chini na kukamilisha uchezaji mzuri wa Barca dakika moja kabla ya mechi kumalizika.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC