
Ndoto
za Mangala kuhamia Ligi Kuu ya England hatimaye zilitimia jana baada ya
kuupiku uhamisho wa Pauni Milioni 30 uliomtoa Rio Ferdinand Leeds
kuhamia Manchester United mwaka 2002.
Mangala,
mwenye umri wa miaka 23, anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na City
baada ya kukubali Mkataba wa miaka mitano na kocha Manuel Pellegrini
anaamini huyo ni moja ya mabeki wa thamani ya juu Ulaya na atadhihirisha
thamani yake uwanjani.
Mfaransa huyo baada ya kukamilisha uhamisho wake amesema; "Mimi ni aina ya mchezaji ambaye naingia uwanjani kushinda,".
"Siachi
kitu chochote, wakati wote napambana hadi mwisho na nina matumaini kwa
desturi yangu huu, tutashinda mataji mengi msimu huu.
"Nina
furaha sasa kwa sababu nitakuwa tayari kuanza maisha mapya. Nitakuwa
tayari kufanya mazoezi tena. Ilikuwa vizuri kwenda mapumziko, lakini
baada ya muda unarudi kazini.
"Ninakwenda
kukimbia kila siku na kufanya mazoezi kwenye gym. Mapumziko ni mazuri,
lakini yakiwa marefu, inakuwia vigumu kurudi vizuri. Nafikiri nitahitaji
muda, ila nitapambana kurudi katika ubora wangu kwa asilimia 100 haraka
iwezekanavyo.
"City
ni klabu kubwa Ulaya. Kwangu, ilikuwa hatua muhimu kuondoka Porto na
kujiunga na Manchester City ili kusonga mbele kimafanikio. Nataka
kushinda mataji na ninaamini nitafanya hivyo,"amesema.