UONGOZI WA SIMBA WAVAMIA BUNJU

UONGOZI wa juu wa klabu ya Simba ukiongozwa na makamu wa rais Gofrey Nyange 'Kaburu' leo umetembelea uwanja wa klabu hiyo uliopo Bunju ambao bado unaendelea na ujenzi wake, Kaburu na sekretalieti nzima ya Simba ilivinjali uwanjani hapo na kushuhudia maendeleo ya ujenzi ya uwanja huo.

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo Kaburu amesema jitihada zao zinahitajika ili kuumalizia uwanja huo na kuanza kutumika, wachezaji wa Simba huenda wakaana kuutumia uwanja huo, endapo Simba itaanza kuutumia uwanja wake huo itakuwa imewapiga bao Yanga ambao wanaendelea kukodi viwanja vya kufanyia mazoezi.


Simba ilianza mpango wake wa kujenga uwanja wake wa kufanyia mazoezi tangia ikiwa chini yake Alhaj Ismail Rage ambaye muda wake wa uongozi umemalizika na sasa uongozi mpya chini yake rais Evans Avea umeanza kazi.