Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MBWANA SAMATTA, THOMAS ULIMWENGU WAWASILI DAR TAYARI KUIKABILI MAMBAZ

WASHAMBULIAJI tegemeo wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu wamewasili Dar es Salaam asubuhi ya leo kujiunga na timu hiyo kwa ajili ya mchezo wa kimataifa dhidi ya Msumbiji ‘Mambas’ mwishoni mwa wiki.

Washambuliaji hao wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) wote wamewasili wakiwa fiti tayari kwa mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Pili na ya mwisho kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Morocco.


Mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, wachezaji hao walisema kwamba wanashukuru wameruhusiwa mapema kuja kujiunga na Stars kwa ajili ya mchezo huo wa Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

“Tunashukuru tumefika salama, tunashukuru kuruhusiwa mapema kuja kwa ajili ya mchezo huu muhimu kwa taifa letu, nasi tunawaahidi Watanzania kupigana kwa nguvu zetu zote kwa kushirikiana na wenzetu waliopo kambini Mbeya, ili kuitoa Msumbiji,”alisema Ulimwengu.

“Mimi nashukuru nimekuja  nikiwa fiti, kama utakumbuka katika mchezo uliopita dhidi ya Zimbabwe nilikuwa majeruhi sikucheza, ila sasa nipo tayari kulipigania taifa langu, naomba Watanzania wajitokeze kwa wingi Jumapili kuja kutupa sapoti,”alisema Samatta kwa upande wake.

Samatta na Ulimwengu waliotua na ndege ya shirika la Misri wakitokea Tunisia ambako TP Mazembe imepiga kambi kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika, walielekea hoteli ya Courtyard katikati ya Jiji baada ya kuwasili JNIA.

Kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kilichopiga kambi Tukuyu mkoani Mbeya, kinatarajiwa kurejea keshokutwa Dar es Salaam kwa maandalizi ya mwisho na Samatta na Ulimwengu wataungana na wenzao siku hiyo.

Kwa sasa wachezaji hao watakuwa wakifanya mazoezi peke yao Dar es Salaam hadi watakapoungana na wenzao Ijumaa kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezeshwa na refa Mahmoud Ashour kutoka Misri.

Mambas nao wanatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Ijumaa wakati mechi ya marudiano itachezwa kati ya Agosti 1 na 3 mwaka huu nchini Msumbiji.

Chanzo Bin Zubeiry

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC