DROGBA AREJEA DARAJANI

Mshambuliaji wa Garatasalay ya Uturuki na Ivory Coast Didier Drogba amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga tena na Chelsea ya England.

Drogba, 36, alishinda makombe 10 akiwa na Chelsea kuanzia mwaka 2004 hadi 2012, na alikuwa mchezaji huru baada ya kuondoka klabu ya Galatasaray ya Uturuki.

Meneja Jose Mourinho, mapema alisema Stamford Bridge ni kama "kwake" mchezaji huyo, Mourinho ameonyesha kufurahishwa kwa kurejea mshambuliaji huyo ambaye anaamini anaweza kuisaidia timu hiyo katika kupachika mabao .


Drogba ameiambia tovuti ya Chelsea kuwa: "Ulikuwa uamuzi rahisi- sikuweza kukataa nafasi ya kufanya kazi tena na Jose."

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI