Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SIMBA SASA HAKUKALIKI, NDUMBARO AMSHIKA PABAYA WAMBURA

Wakati Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba jana imetangaza rasmi kuwatema wanachama saba waliokuwa wanawania nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, wengine watano wameandika barua za kujiondoa kwenye kinyang'anyro hicho, imeelezwa.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo, Damas Ndumbaro, aliwataja wagombea walioondolewa katika mchakato wa uchaguzi kwa sababu ya sifa za kutokuwa na elimu ya kidato cha nne iliyothibitishwa na Baraza la Mitihani nchini kama ilivyoelezwa katika katiba ibara ya 26(2) ni pamoja na George Wakuganda, Salim Jazaar na Sueliman Dewji.

Ndumbaro aliwataja wagombea waliotema kutokana na uanachama wao kutotimia miaka mitatu na kuruhusiwa kugombea kwa mujibu wa ibara ya 26( 6) cha katiba ya Simba ni Emmanuel Kazimoto, Ahmed Mlanzi, Omary Omary na Ramson Rutiginga.

Aliwataja wagombea waliojiondoa kwa sababu za kifamilia na kuwasilisha barua kwa kamati hiyo ni Juma Pinto, Asha Kigundula, na Hussein Simba waliokuwa wanawania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji na kwenye nafasi ya Makamu wa Rais ni Joseph Itang'are na Wilbroad Mayage.

Aliwataja wagombea waliopitishwa kuwa ni Evans Aveva na Andrew Tupa (Urais) na Geofrey Nyange 'Kaburu', Swedy Mkwabi, Jamhuri Kihwelo 'Julio' na Bundala Kaburwa wanaowania nafasi ya Makamu wa Rais.

Nafasi ya Ujumbe ni Ally Suru, Abdulhamid Mshangama, Alfred Elia, Chano Almasi, Amina Poyo, Asha Muhaji, Collins Frisch, Ally Chaurembo, Daniel Manembe, Khamis Mkoma, Iddi Mkambala, Addi Kajuna, Jasmin Badar, Juma Mussa, Maulid Abdallah, Rodney Chiduo, Said Kubenea, Said Pamba, Said Tully na Yasin Mwete.

Hata hivyo, Ndumbaro alisema kwamba hiyo si orodha ya mwisho ya wagombea kwa sababu sasa hivi kamati yake inapeleka majina hayo katika Kamati ya Maadili kwa ajili ya kuyapitisha.

"Orodha ya mwisho itatolewa Juni 23, huenda majina mengine kati ya haya yanaweza kukumbwa na Kamati ya Maadili ya TFF au mamlaka husika za dola ambazo bado zinaendelea na kazi zao, tunachotaka haki itendeke," alisema Ndumbaro.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na kamati hiyo, kuanzia leo hadi Juni 7 ni muda wa Kamati ya Rufaa kukutana kujadili pingamizi au rufaa zitakazokuwa zimewasilishwa.

Wambura alikufa 2010-ndumbaro

Kamati hiyo pia imemtaka aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Urais ya klabu hiyo, Michael Wambura, kuwaomba radhi kutokana na kitendo chake cha kuwadhalilisha na kueleza kwamba Katibu huyo wa zamani wa Chama cha Soka nchini (FAT sasa TFF) 'alikushakufa' tangu mwaka 2010.

Ndumbaro, alisema mgombea huyo ameidhalilisha kamati hiyo kwa kueleza kwamba imekula rushwa ya ngono na fedha ili kupitisha majina ya baadhi ya wanachama waliokuwa wanawania nafasi za uongozi kwenye klabu hiyo.

Ndumbaro alisema kwamba kauli aliyoitoa Wambura dhidi ya Kamati ya Uchaguzi imewadhalilisha na inamtaka awaombe radhi kwa kutumia njia ile ile aliyoitumia kutoa 'kashfa' na endapo hatafanya hivyo watamchukulia hatua.

"Wambura ni bingwa wa kwenda mahakamani, Simba ilimpitisha 2010, akagonga kisiki TFF kwa kumuondoa, kuipeleka Simba mahakamani ni sawa na kifo na kwa sababu alishakufa, kamati imemzika kwa kuamini kwamba alishakufa," alisema Ndumbaro.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC