NEYMAR AUMIA MAZOEZINI, LAKINI........

MASHABIKI na wapenzi wa soka Brazil jana waliingiwa hofu kufuatia mshambuliaji wao nyota, Neymar kukaa chini mazoezini akiugulia maumivu ya kifundo cha mguu na kuzua hofu juu ya uimara wake keuelekea Kombe la Dunia.


Nyota huyo wa Barcelona aliumia enka wakati wa mazoezi Selecao nje ya Rio de Janeiro na kumlazimisha kupata huduma ya kwanza uwanjani.


Hata hivyo, baada ya dakika kadhaa za kutibiwa, mchezaji huyo ambaye amepamba bang la tangazo la Kombe la Dunia mwaka huu, aliinuka na kuendelea na mazoezi.

Neymar aliinuka baada ya kupatiwa huduma ya kwanza na kurudi kuendelea na mazoezi, kujiandaa na mchezo wa ufunguzi dhidi ya Croatia keshokutwa