
Pia Yanga watakutana nayo Agosti katika mechi ya ngao ya hisani, mwaka jana timu hizo zilikuatana katika mechi kama hiyo na Azam ilikubali kichapo cha bao 1-0 hivyo mwaka huu haitakubali kufungwa na ndio maana wameingia kambini upesi.
Aidha Azam mwakani itashiriki ligi ya mabingwa barani Afrika hivyo inaweza kujikuta inapangiwa na miamba kama TP Mazembe, Al Ahly au Enyimba International, kuanza mazoezi mapema kunapelekea ufiti kwa nyota wake na kufanya vizuri katika ligi na michuano ya kimataifa.
Mazoezi hayo yamefanyika kwenye uwanja wake uliopo chamazi jijini Dar es salaam chini ya kocha msaidizi Kalimangonga Ongala, Ibrahim Shikanda, Iddy Cheche pamoja na kocha wa Makipa Iddy Abubakari.
Kocha mkuu Joseph Omog anatarajia kujiunga na timu tarehe 20/6/2014. Azam Fc Mapinduzi ya kweli katika soka
