
NATOA angalizo kwa taasisi ya kupambana na rushwa nchini Takukuru kuwa macho na uchaguzi wa klabu ya Simba unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Tayari uchaguzi huo umeonyesha kuwepo kwa vitendo vya rushwa vinavyodaiwa kufanywa na baadhi ya wagombea, wapo baadhi ya wagombea wamekuwa wakitumia kuwapa wanachama fedha ili wawachague.
Lakini pia wapo wagombea wanaotoa rushwa kwa njia ya kuahidi kufanya usajili wa kutisha ama kumleta nyota fulani katiika klabu hiyo ili mradi akubalike kwa wanachama.
Takukuru kama hamjakuwa makini basi vitendo vya rushwa vitazidi kushamili hapa nchini, aidha pia baadhi ya wagombea wamekuwa wakitoa fedha kwa wanachama wa klabu hiyo kupitia matawi yao na kuwaahidi kuwajengea mazingira safi pindi tu akiingia madarakani.

Badala ya kushindana kwa sera wamekuwa wakitumia nafasi nyingine ya kugawa fedha kwa wanachama hasa wale wenye njaa huku wakidiriki kuwaponda wagombea wenzao.
Nawaambia wanachama wa Simba msikubali kurubuniwa kwa fedha kidogo wala usimuone mgombea mwenye fedha ndito anafaa kuiongoza Simba, Simba ni mali ya watu wote iwe masikini au tajiri.
Unapokubali kununuliwa kwa fedha ina maana umeiweka shakani klabu yako kwa kipindi chote cha utawala wa kiongozi aliyekununua, pia hautaweza kumpinga kwa lolote hata kama anaboronga kwa vile umenunuliwa.

Wanachama waliandamana kwa majembe, shoka, nyundo, panga nk kufyeka uwanja wakati kumbe kuna matajiri wamejificha pembeni wanangoja uchaguzi, viongozi wa namna hii hawafai na tuwaogope kama ukoma.
Nakumbuka kauli ya baba wa taifa hayati Julius Kambarage Nyerere alisema 'Ikulu hakununuliwi' hiyo ina maana mgombea anayetaka kuongoza Simba kwa kutoa fedha hafai..tuonane wiki ijayo