Ruka hadi kwenye maudhui makuu

YANGA YAIKARIBIA AZAM KILELENI

Yanga iliongeza presha dhidi ya vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bar, Azam FC, wakati walipoibwaga Kagera Sugar kwa magoli 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kubakisha pointi moja kuwashika vinara.

Hata hivyo, Azam FC yenye pointi 53 wana nafasi ya kurejesha pengo la pointi kileleni kuwa pointi nne tena kwa ushindi katika mechi moja yao ya mkononi watakayoicheza leo dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini baada ya kuahirishwa jana kutokana na uwanja huo kujaa maji kufuatia mvua kubwa zilizonyesha.

Refa Isihaka Shirikisho kutoka Tanga kwa kushirikiana na wasaidizi wake Hassan Xani wa Arusha, Agnes Pantaleo wa Arusha, Simon Mbelwa wa Pwani na Kamisaa Isabela Kapela wa Dar ndiyo walioukagua uwanja wa Mabatini na kufanya maamuzi ya kuahirisha mchezo huo.


Kwenye Uwanja wa Taifa, mabingwa Yanga walipata goli la kuongoza mapema katika dakika ya tatu kupitia mshambuliaji Mganda Hamis Kiiza aliyeitendea haki krosi murua iliyomiminwa kwenye boksi la Kagera Sugar na winga Mrisho Ngasa ambaye aliwahi pia kuichezea timu hiyo pekee Ligi Kuu kutoka mkoa wa Kagera.

Yanga ambao wako hatarini kuachia taji lao kwa Azam, walipata goli la pili katika dakika ya 36 likifungwa na mshambuliaji Mrundi Didier Kavumbagu aliyemlamba chenga kipa Agatony Antony baada ya kupokea kwa kifua krosi safi ndani ya boksi iliyotolewa na winga Simon Msuva aliyepenyezewa mpira na Ngasa. Mpikaji huyo wa goli la kwanza alikimbia na mpira kwa kasi kutoka katikati ya uwanja lakini alipokaribia boksi la Kagera akatoa pasi pembeni kwa Msuva.

Hadi mapumziko, Yanga walikuwa wakiongoza 2-0 lakini wageni ndiyo waliofanya mashambulizi mengi zaidi katika kipindi cha kwanza lakini kipa Deogratius Munishi 'Dida' aliiokoa Yanga kuoga mvua ya magoli baada ya kuokoa michomo mingi ya hatari.

Katika mechi iliyohudhuriwa na mashabiki wachache, Kiiza alikuwa na fursa ya kuifungia goli la tatu katika dakika ya 50 lakini alipiga shuti nje wakati akimalizia mpira wa krosi kali ya Msuva ndani ya sita.

Daudi Jumanne alipatia Kagera Sugar goli la kufutia machozi katika dakika ya 61 baada ya kuunasa mpira uliookolea kizembe kwa kichwa na beki wa pembeni Oscar Joshua na kuifanya Yanga itaabike katika muda wote uliokuwa umebaki kuwazuia Wakatamiwa hao wa Kagera kusawazisha.

Beki wa Kagera Sugar, Ernest Mwalupani alikuwa na bahati kutotolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya 64 baada ya kumsukuma refa Maalim Abbas akimtuhumu kuibeba Yanga lakini mwamuzi huyo kutoka Rukwa aliishia kumwonya kwa kadi ya njano.

Msuva aliinyima Yanga goli jingine katika dakika ya 85 wakati alipopiga mpira nje akiwa ndani ya sita.

Mwishoni mwa mechi wachezaji wa Yanga hasa Kavumbagu walitaka kuzichapa na mabeki wa Kagera lakini marefa wakawaamua na muda mfupi baadaye polisi wakafika kuhakikisha kila mmoja anaondoka salama uwanjani humo.

Yanga: Deogratius Munishi, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Mbuyu Twite, Frank Domayo, Simon Msuva, Hassan Dilunga, Didier Kavumbagu, Mrisho Ngasa na Hamis Kiiza.

Kagera Sugar: Agatony Antony, Salum Kanoni, Mohamed Hussein, Ernest Mwalupani, Maregesi Mwangwa, George Kavila, Benjamin Asukile, Daudi Jumanne, Adam Kingwande, Themi Felix na Paul Ngwai.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC