Ruka hadi kwenye maudhui makuu

YANGA ITAIFUNGA SIMBA KESHO BILA OKWI, NIYONZIMA

YANGA SC imeingiza wachezaji 20 kambini eneo la Bahari Beach kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu, Simba SC kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kukamilisha msimu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa taarifa ya kwenye tovuti ya klabu hiyo jana, wachezaji walioingia kambini ni makipa; Deogratius Munishi ‘Dida’ na Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Ibrahim Job, Rajab Zahir, Kevin Yondan na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, wakati viungo ni Frank Domayo, Hassan Dilunga, Salum Telela, Hamisi Thabit na Nizar Khalfan na washambuliaji ni Didier Kavumbagu, Mrisho Ngassa, Jerry Tegete, Hamisi Kiiza, Hussein Javu na Simon Msuva.


Bado hazijulikani sababu za wachezaji Juma Kaseja,Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima, Athumani Iddi ‘Chuji’ na David Luhende kutokuwa kambini tangu baada ya mechi na JKT Mgambo Yanga wakilala 2-1 Tanga.

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm amekaririwa na tovuti hiyo akisema vijana wake wapo katika hali nzuri kuelekea mchezo wa Jumamosi, kwani hakuna majeruhi hata mmoja kati yao.

Amewasifu wanazidi kuonyesha mabadiliko makubwa kiuchezaji, mafunzo yake wanaonekana kuyaelewa vizuri hivyo kikubwa anaomba waendelee kuwa katika hali nzuri kuelekea mchezo na ana imani kikosi chake kitaibuka na ushindi.

“Nina uzoefu na michezo ya watani wa jadi, huwa inakua migumu kwa kila timu kutokana na kila timu kutaka kuonyesha wapenzi, washabiki na wanachama wake kuwa wako vizuri, Simba ni timu nzuri, lakini bado sioni kikwazo cha kutuzuia tusiibuke na ushindi katika mchezo huo,’alisema.

Leo jioni kikosi kitafanya mazoezi katika Uwanja wa Bko Beach Veterani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo huo.
Yanga SC imeshindwa kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu, baada ya kuzidiwa kete na Azam FC iliyofikisha pointi 59 ikiwa na mechi moja mkononi ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yeyote.

Yanga SC itafikisha pointi 58 ikifanikiwa kuifunga Simba SC ambayo imeweka kambi visiwani Zanzibar tangu jana kwa ajili ya mchezo huo.

Chanzo Bin Zubeiry

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC