Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SWEBE AWALAANI WAUZA SURA KWENYE SANAA

Na Regina Mkonde

Msanii mkongwe wa hapa nchini kutoka kundi la Kaole Kwanza maarufu kama Swebe Santana (Pichani) alisema kuwa kazi nyingi za sanaa zinashindwa kuendelea na kufahamika kimataifa kwa kuendekeza kuuza sura badala ya kufanya sanaa.

Swebe aliongeza kuwa wasanii wengi na wadau wengi wa sanaa hapa nchini hawaangalii uwezo na kipaji cha mtu katika sanaa bali wanachoangalia ni umaarufu na sura ya mtu huku wenye vipaji vyao kukosa nafasi.


Tatizo lipo kwa baadhi ya maproducer feki na wasambazaji feki ambao wapo kwa ajili ya watu wao binafsi utakuta mara kwa mara wanawapa nafasi ya kuigiza watu maarufu ambao hawana vipaji vya kuigiza pia wanachokifanya ni kutengeneza mastaa wao.Alisema Swebe.

Wapo baadhi ya maproducer walitubania enzi hizo wakidhani kuwa watafanikiwa lakini mwisho wa siku hawana issue na wamefulia isitoshe wameharibu na kuua hadhi ya sanaa. Aliongeza msanii huyo.

Miaka ya nyuma sanaa ya Tanzania ilikuwa ina maendeleo mazuri lakini kwa sasa imefulia na hii yote inasababishwa na baadhi ya wasanii kutokuwa wabunifu badala yake wanaiga kazi za watu wa nje, utakuta msanii anaangalia kazi za nje kama za Wanageria wahindi wazungu n.k kisha anaiga idea yake na kujifanya ameibuni kazi mwenyewe.

Hivi sasa hatuna wasanii bora na wenye wito kama zamani sasa hivi watu wengi hukimbilia kuigiza hata kama hawana vipaji ili mradi wapate umaarufu na mafanikio ya haraka.

Miaka ya nyuma wasanii walikuwa na wito wa kazi za sanaa hawakujali maslahi ya pesa ila walio wengi sasa wanaangalia maslahi ya pesa badala ya sanaa kwa ufupi hivi sasa sanaa imekuwa biashara ambayo kila mtu anataka kuifanya.

Kuuza sura ndiyo sababu iliyopelekea maendeleo ya sanaa kuwa duni kuna baadhi ya maproducer wanaangalia watu maarufu wenye mvuto badala ya kuwaangalia wenye vipaji vya sanaa.

Uongo kwenye tasnia ya filamu hivi sasa umekuwa fasheni wasanii wengi ni waongo hawana ushirikiano na hawapendani pia ndiyo maana utakuta wengi wao hufanya kazi na watu maarufu tu na kuacha wasanii chipukizi fani zao zikipotea.

Mara nyingi sana ukiangalia filamu za kibongo utakuta wasanii ni wale wale wa kila siku ambao ni mastaa wale chipukizi hawapewi kipaumbele kabisa na kama msanii mchanga akitaka kupata nafasi lazima atoe rushwa kidogo ili apate nafasi,swala hili linafanyika kwa baadhi ya wasanii na wadau wa sanaa wengi hapa nchini.Alisema Swebe.

Miaka kadhaa iliyopita Tanzania ilikuwa inafanya vizuri kwenye sanaa na ikapata fursa ya kufanya kazi na wasanii maarufu kutoka nchini Nigeria na ikafahamika pia ila kwa sasa desturi hii imekufa na sanaa yetu kuporomoka.

Naweza sema kwamba Marehemu Kanumba aliondoka na sanaa ya Tanzania sababu yeye enzi za uhai wake alikuwa kipaumbele kuitangaza nchi yetu kwa kushirikiana na wasanii kutoka nje ya Tanzania ila kwa sasa hakuna aliyethubutu kufanya jambo kama hilo.

Licha ya hivyo wasanii wakubwa hawawapi nafasi watoto wadogo na wasanii wachanga kama watoto wangekluwa wanapewa nafasi hivi sasa nchi yetu ingekuwa na wasanii mashughuli duniani.

Mavazi pia yamekuwa chachu ya kushusha kiwango cha sanaa sababu siyo wadau wote wanaopenda kuangalia picha za wasanii wanaovaa nguo fupi wapo watu wenye heshima zao ambao wanapenda kununua filamu zenye maadili kuanzia kwernye mavazi n.k hali hii inachochea soko la filamu kushuka sababu wadau hawanunui kazi zao.

Kuiga kazi za nje pia imekuwa chachu ya sanaa kudorola mtu anaona bora akakodi Cd badala ya kununua sababu kazi ya sanaa inakua ladha haina na ubora pia.

Ni bora wasanii tuwe na ushirikiano ili tukuze sanaa yetu tuachane na uuzaji wa sura kujuana ili sanaa yetu ipande chati kimataifa.Alisema msanii huyo kutoka kundi la Kaole Kwanza ambalo hapo awali lilikuwa linafahamika kwa jina la Kaole Sanaa Group.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Ngao ya Jamii sasa ni Simba na Yanga

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limebadilisha kanuni za mashindano za Ngao ya Jamii kutoka timu nne na sasa utaratibu utakuwa kama zamani. Bingwa wa Ligi Kuu bara atacheza na mshindi wa kombe la CRDB Cup "CRDB Federation Cup, na endapo kama bingwa wa ligi na CRDB atakuwa ni mmoja basi mshindi wa pili kwenye Ligi Kuu ya NBC atacheza mchezo wa ufunguzi wa ligi yaani Ngao ya Jamii.  Hivyo ni rasmi ufunguzi wa wa ligi kuu mchezo  wa "Ngao ya Jamii msimu huu 2025-2026 ni Yanga na Simba watakutana.

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...