Ruka hadi kwenye maudhui makuu

STURRIDGE HUENDA AKAIKOSA NORWICH

Daniel Sturridge

Straika wa Liverpool Daniel Sturridge huenda asisafiri na viongozi hao wa Ligi ya Premia kwenda Norwich City Jumapili kutokana na jeraha la misuli.

Fowadi huyo wa Uingereza alilazimika kuondoka uwanjani dakika ya 66 wakati wa ushindi wao wa 3-2 dhidi ya wapinzani wao ligini Manchester City mnamo Jumapili kutokana na kilichoonekana kuwa jeraha la misuli ya paja.

"Sturridge amefanyiwa uchunguzi zaidi na matabibu wa klabu Melwood na jeraha ndogo lilionekana baada ya uchunguzi huo,” Liverpool walisema kupitia taarifa kwenye tovuti yao (wwww.liverpoolfc.com) mnamo Jumatano.

Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea na Manchester City mwenye umri wa miaka 24 amefunga mabao 20 msimu huu na kuunda ushirika wa kufana na strika wa Uruguay Luis Suarez ambao umefanya Liverpool kukaribia sana kushinda taji lao la kwanza la ligi tangu 1990.


Liverpool wanaongoza wakiwa na alama 77 kutoka mechi 34, mbili mbele ya Chelsea, huku City wakiwa na 71 baada ya sare ya 2-2 na Sunderland Jumatano lakini wakiwa na mechi moja hawajacheza.
Baada ya kuzuru Norwich wanaokabiliwa na hatari ya kushushwa ngazi,

Liverpool watakuwa wenyeji wa wapinzani wao katika kuwania taji Chelsea, kisha wakutane na Crystal Palace ugenini kabla ya kumaliza kampeni yao msimu huu kwa kukabiliana na Newcastle United nyumbani.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Ngao ya Jamii sasa ni Simba na Yanga

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limebadilisha kanuni za mashindano za Ngao ya Jamii kutoka timu nne na sasa utaratibu utakuwa kama zamani. Bingwa wa Ligi Kuu bara atacheza na mshindi wa kombe la CRDB Cup "CRDB Federation Cup, na endapo kama bingwa wa ligi na CRDB atakuwa ni mmoja basi mshindi wa pili kwenye Ligi Kuu ya NBC atacheza mchezo wa ufunguzi wa ligi yaani Ngao ya Jamii.  Hivyo ni rasmi ufunguzi wa wa ligi kuu mchezo  wa "Ngao ya Jamii msimu huu 2025-2026 ni Yanga na Simba watakutana.

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...