Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SIMBA KIMEELEWEKA TAYARI KUIUA YANGA JUMAMOSI

Mjumbe wa kuteuliwa wa Kamati ya Utendaji ya Simba na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo,Zacharia Hanspoppe.

Mjumbe wa kuteuliwa wa Kamati ya Utendaji ya Simba na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hanspoppe jana amesaidia fedha za mishahara ya wachezaji ambao waligoma kwenda Zanzibar bila ya kulipwa.

Mjumbe huyo ametoa zaidi ya Sh. milioni 30 kusaidia malipo hayo kutokana na wachezaji kukataa kwenda Zanzibar bila kulipwa mishahara yao na posho kwa ajili ya kujiandaa na mechi yao ya kukamilisha ratiba dhidi ya Yanga itakayofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa.


Habari ambazo gazeti hili imezipata zimeeleza kuwa baada ya leo asubuhi wachezaji kumaliza mazoezi walitakiwa kuelekea bandarini lakini nyota hao waligoma mpaka madai yao yalipofanyiwa kazi.

Kufuatia hali hiyo, kikosi cha nyota 18 walioteuliwa kwenda Zanzibar kililazimika kuahirisha safari asubuhi na badala yake kimeondoka boti ya saa tisa mchana.

"Hanspoppe ndiyo ameokoa jahazi wachezaji waligoma hadi walipolipwa...aibu sana," kilisema chanzo chetu.

Fedha hizo zilizotolewa wamelipwa wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi mshahara wa mwezi uliopita.

Awali benchi la ufundi lilipendekeza timu iingie kambini juzi Jumanne lakini ilishindikana kutokana na kukosa fedha.

Hanspoppe amekataa kuzungumzia hali hiyo iliyotokea ndani ya klabu.

Wachezaji walioondoka kuelekea kambini Zanzibar ni pamoja na Ivo Mapunda, Yaw Berko, William Lucian, Issa Rashid, Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Haroun Chanongo, Amri Kiemba, Amissi Tambwe, Said Ndembla na Ramadhan Singano.

Nyota wengine ni Nassor Masoud 'Chollo', Henry Joseph, Ramadhan Chombo ' Redondo', Uhuru Selemani, Awadh Juma na Zahor Pazi.

Simba na Yanga zinawania kushinda mechi hiyo ili kulinda heshima baada ya bingwa wa msimu huu, Azam FC, kuwa ameshapatikana.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa