Ruka hadi kwenye maudhui makuu

REAL MADRID YAILAZA BAYERN MUNICH 1-0

Mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos (kulia) anaruka hewani kuugonga mpira katika UEFA Champions League hiyo jana. 

Japo ni kwa ushindi finyu wa bao 1 bila - Real Madrid wamejiwekea akiba nzuri kibindoni na ndiyo watakayoendeleza nayo kampeni yake ya kuwania kuipokonywa ubingwa wa Champions league Bayern.
Karim Benzema ndie alitingisha wavu wa Bayern mapema katika kipindi cha kwanza.

Mashambulio ya Christino Ronaldo yalikuwa yakisisimua lakini hayakuzaa matunda zaidi kwa Real. Juhudi za Bayern za kukomboa bao hilo zilizimwa kabisa - hivyo kuiwezesha Real kuendeleza rekodi yao ya kutoshindwa nyumbani kufikia mechi 18 .


Bayern sasa itajitahidi itumie vilivyo morali wa mashabiki wao nyumbani hapo jumanne kuwageuzia kibao Real. Mshindi atakutana na Chelsea AU Atletico Madrid, ikitegemea matokeo ya mechi yao ya Jumatano katika raundi yao ya pili ya nusu fainali hiyo.

Na kocha Jose Mourinho yu matatani tena... Ni miongoni mwa wafanyikazi watatu wa-Chelsea waliofunguliwa mashtaka na FA kwa madai ya kuonesha ukosefu wa nidhamu wakati wa mechi iliyowafedhehesha pale walipofungwa na Sunderland 2-1 , timu ambayo iko mkiani mwa league ya Premier.

Baada ya mechi hiyo Mourinho alitoa 'pongezi' tele hasa kwa refa Mike Dean na kumtaja kuwa mtu wa kustaajabisha sana kwa jinsi alvyoendesha mechi hiyo...na pia akampongeza mkuu wa bodi ya marefa Mike Riley- Sasa matamshi hayo yamechukuliwa kama kejeli za kuwashusha hadhi aliyowataja.

Amepewa mpaka 28 April kujibu mashtaka hayo. Wenzake mchezaji Ramires anasemekana alitishia kutumia nguvu uwanjani hasa pale alipobishana kwa sababu ya penalty iliyopewa Sunderland huku meneja msaidizi Faria pia anadaiwa alitumia lugha isiyostahili.

Si mara ya kwanza kocha Morihno anajikuta matatani kwa sababu ya tabia yake ya kutupa vijembe vya maneno kwa mahasimu wake lakini wengi wa wafuasi wake huvutiwa sana na mafumbo yake.

Tumalizie kwa mashindano ya klabu bora cha Voliboli ya wanawake wa Afrika yanayoendelea huko Tunisa.
Timu za Kenya zimekuwa zikifanya vizuri sana- Mojaapo ni bigwa watetezi magereza, imezishinda timu walizokuwa nao katika kundi moja za Aljeria , Cameroon na Misri na pia kushinda mechi yao ya jana ya robo fainali kwa seti tatu kwa bila dhidi ya timu kutoka Tunisia.Timu hiyo ya magereza wamelishinda kombe hilo mara 5 , kwa miaka minne ikiwa mfululizo.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC