Ruka hadi kwenye maudhui makuu

PHLPS KUOGELEA TENA


Michael Phelps kurejea katika mashindano ya uogeleaji
Bingwa wa dunia katika mashindano ya uogeleaji, Michael Phelps anapania kurejea tena katika ulingo wa uogeleaji hivi


karibuni. Mkufunzi wake Bob Bowman anasema mwogeleaji huyo angali ana muda mrefu wa kupiga mbizi majini kabla ya kustaafu.

Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 28 ambaye ameshinda medali 22 ya Olimpiki, anatarajiwa kushiriki mashindano ya Arizona mwishoni mwa mwezi huu wa Aprili.

Phelps alistaafu baada ya kushinda medali yake ya 18 ya dhahabu ya olimpiki huko London.
Phelps anayefahamika kama The Baltimore Bullet ndiye anayeshikilia rekodi ya kuwa mwanaspoti aliyewahi kushinda nishani nyingi zaidi za dhahabu

katika mashindano moja alipotwaa ubingwa katika mashindano 8 ya uogeleaji huko Beijing mwaka wa 2008.
Michael Phelps kurejea katika mashindano ya uogeleaji
Bowman amesema kuwa Phelps atashiriki katika mashindano tatu ya uogeleaji ile ya mita 100 mtindo wa butterfly mita 50m na 100m mtindo wa freestyle
katika mashindano hayo yatakayofanyika tarehe 24 mwezi huu.

Kocha Bob Bowman alikuwa ameiambia BBC mwaka uliopita kuwa Phelps anapania kushinda medali zaidi za katika mashindano ya olimpiki ya Rio de Janeiro Brazil mwaka wa 2016.
Phelps alirejea mazoezini mwaka uliopita na sasa amekamilisha muda wa makataa ya miezi 6 ya uchunguzi wa utumizi wa madawa na sasa yu tayari kwa mashindano .

Muogeleaji huyo Stadi sasa atapimana nguvu na waogeleaji nyota Ryan Lochte na Katie Ledecky katika mashindano hayo ya Mesa.
Phelps si mwogelaji wa kwanza kurejea mashindanoni baada ya kustaafu.
Mwaka wa 2012 muogeleaji Ian Thorpe, kutoka Australia alijaribu kurejea mashindanoni lakini akashindwa .

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC