Ruka hadi kwenye maudhui makuu

RAIS KIKWETE KUWEKA HISTORIA KESHO DODOMA, APANGA KUHUTUBIA MBELE YA WATANGULIZI WAKE

Rais Jakaya Kikwete kesho ataambatana na ujumbe mzito wa marais wastaafu wa pande zote za Muungano, wake wa waasisi wa taifa na mawaziri wakuu wastaafu atakapokwenda kuzindua Bunge Maalumu la Katiba.

Hatua ya Rais kuambatana na ujumbe huo imepongezwa na viongozi wa vyama vikuu vya upinzani nchini, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na mwenzake wa Chadema, Freeman Mbowe.

Mbali na viongozi hao, Rais Kikwete pia ataambatana na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad.


Wanaotarajiwa kuwamo katika msafara huo ni Rais wa pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi, Rais wa tatu, Benjamin Mkapa na marais wastaafu wa Zanzibar, Dk Salmin Amour na Amani Abeid Karume, Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume.

Miongoni mwa mawaziri wakuu wastaafu wanaotarajiwa kuwamo ni pamoja na Jaji Joseph Warioba, ambaye juzi aliwasilisha bungeni hapo Rasimu ya Katiba kwa kutoa hotuba iliyoliteka Bunge kwa jinsi alivyofafanua mambo mengi yenye utata kuhusu muundo wa Muungano.

Mawaziri wakuu wengine ni Cleopa Msuya, John Malecela, Dk Salim Ahmed Salim, Frederick Sumaye pamoja na Edward Lowassa na Mizengo Pinda ambao ni wajumbe wa bunge hilo.

Wengine walioalikwa ni mabalozi wa nchi mbalimbali, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, viongozi wa dini, vyama vya wafanyakazi, vyama vya siasa, wafugaji, wakulima, wavuvi na wawakilishi wa sekta binafsi.

Katibu wa Bunge Maalumu la Katiba, Yahaya Khamis Hamad aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Rais Kikwete atahutubia Bunge hilo kwa mujibu wa Kanuni ya 75 (1).

Rais Kikwete atapokewa katika Viwanja vya Bunge na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta na baadaye kukagua gwaride maalumu kabla ya kuhutubia Bunge kuanzia saa 10:00 jioni.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana, baada ya Rais kuhutubia saa 11:35 jioni, aliyekuwa mwenyekiti wa muda wa bunge hilo, Pandu Ameir Kificho atatoa neno la shukurani kabla ya Rais kupiga picha za kumbukumbu na wajumbe wa Bunge hilo.

Suala la hotuba ya Rais Kikwete limekuwa sehemu ya mjadala katika Bunge hilo kutokana na baadhi ya wajumbe kuhoji sababu za Jaji Warioba kuwasilisha Rasimu kabla ya Rais kuzindua Bunge kwa mujibu wa kanuni.

Mjadala huo uliwafanya baadhi ya wajumbe kumzuia Jaji Warioba Jumatatu iliyopita kuwasilisha rasimu hiyo kama ilivyokuwa imepangwa hadi kilipofanyika kikao cha maridhiano siku hiyohiyo usiku na kufikia mwafaka kwamba Mwenyekiti huyo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba awasilishe Rasimu juzi na Rais ahutubie kesho.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Ngao ya Jamii sasa ni Simba na Yanga

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limebadilisha kanuni za mashindano za Ngao ya Jamii kutoka timu nne na sasa utaratibu utakuwa kama zamani. Bingwa wa Ligi Kuu bara atacheza na mshindi wa kombe la CRDB Cup "CRDB Federation Cup, na endapo kama bingwa wa ligi na CRDB atakuwa ni mmoja basi mshindi wa pili kwenye Ligi Kuu ya NBC atacheza mchezo wa ufunguzi wa ligi yaani Ngao ya Jamii.  Hivyo ni rasmi ufunguzi wa wa ligi kuu mchezo  wa "Ngao ya Jamii msimu huu 2025-2026 ni Yanga na Simba watakutana.

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...