MO FARAH ATETEA MAAMUZI YAKE

Mo Farah akiwa na Gebreselasie
Mwanariadha wa Uingereza, mzaliwa wa Somalia Mo Farah, amekariri kuwa alifanya uamuzi bora kushiriki katika mashindano kadhaa ya barabarani kabla ya kushiriki katika mbio za London Marathon mwezi ujao.
Farah atakuwa miongoni mwa wanariadha watakaoshiriki katika mbio za kilomita ishirini na moja mjini New York Jumapili hii.

Mwanariadha mashuhuri wa Ethiopa, Haile Gebrselassie alikuwa amesema ni mapema sana kwa Farah mwenye umri wa miaka 30 kushiriki katika mbio hizo za marathon, na badala yake kutoa ushauri kwake kuipa mashindano ya uwanjani nafasi ya kwanza.

Mo Farah wakati wa mashindano ya mbio za dunia mjini Moscow