Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MESSI KULIPWA ZAIDI DUNIANI

KLABU ya Barcelona itamfanya Lionel Messi kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani, kwa kumpa mshindi huyo wa Ballon d'Or nne mshahara wa zaidi ya Pauni 335,000 kwa wiki.

Hiyo ni ahadi ya rais wa klabu hiyo, Josep Maria Bartomeu inayokuja siku mbili tu baada ya nyota huyo wa Argentina kupiga hat-trick Barca ikiifunga Real Madrid na kurejea kwenye mbio za ubingwa.

"Wote tunataka Messi awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani na hilo ndilo tunalolifanyia kazi kwa sasa,"alisema Bartomeu. "Hadi sasa tunaelekeza fikra zetu kwenye mashindano tunayoshiriki, lakini itatokea karibuni,"
.

"Hakuna hapa anayetaka Messi auzwe. Huwezi kumuuza Leo. Alikuja hapa akiwa ana umri wa miaka 13 na ni mmoja wa wachezaji wetu.'

Barcelona ilitoa ofa ya kwanza kwa baba yake Messi ambaye pia ni wakala wake, Jorge, mapema mwaka huu na inafahamika ofa hiyo imefanyia marekebisho pia kipengele cha klabu kumiliki asilimia 100 ya haki ya matumizi ya picha ya mchezaji huyo, ambayo ilikuwa haimpendezi mfungaji huyo wa kihistoria wa timu hiyo.

Rais huyo mpya anakabiliwa na presha ya kuwaridhisha mashabiki kwa kufanya wanachokipenda katika miezi yake sita ya mwanzo na jambo kubwa ni suala la Messi, ambaye Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2018.

Dili hilo linatarajiwa kujadili wakati Jorge Messi atakapoketi chini na Bartomeu kabla ya fainali ya Kombe la Mfalme Aprili 16, na kuongeza mwaka mmoja katikamkataba wa mchezaji huyo ili umalizike 2019 na atampiku Cristiano Ronaldo kwa mshahara akilipwa Pauni Milioni 17.5 kwa mwaka, ambazo ni sawa na Pauni 336,000 kwa wiki.

Pamoja na kumuongezea mshahara ampiku Ronaldo, pia Barca itamruhusu Messi amiliki haki ya matumizi ya picha yake kwa asilimia 100.  Ronaldo kwa sasa anaingiza zaidi ya Messi, lakini Real Madrid inamiliki asilimia 50 ya haki za matumizi ya picha yake

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC