Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MABEKI WANANIKAMIA SANA- OKWI

Ukame  wa kucheka na nyavu unamtesa mshambuliaji wa Kimataifa wa Yanga kutoka Uganda, Emmanuel Okwi, lakini amejitetea kuwa bado kiwango chake cha kucheza soka kiko juu licha ya kutofunga mabao kwenye mechi za Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara inayoendelea.

Yanga ilimsajili Okwi kwa gharama ya zaidi ya milioni 100 akitokea SC Villa ya Uganda ambayo ilipewa kibali cha kumtumia kufuatia kutofautiana na klabu yale ya Etoile Sportive du Sahel ya Tunisia.

Okwi alifunga bao moja wakati mabingwa hao watetezi wakipata ushindi wa 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting na akafunga tena kwa penalti walipokuwa Alexandria wakirudiana na Al Ahly kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika mapema mwezi huu.

Akizungumza Okwi, alisema kuwa anapokuwa uwanjani kila mchezaji wa timu pinzani anajipanga kumzuia yeye ili asiweze kuutawala mchezo.

Okwi ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) alisema licha ya kutofunga, mchango wake kwenye timu unaonekana na anafurahia kuona Yanga bado ina uwezo wa kutetea ubingwa msimu huu.

Alisema ligi ni ngumu lakini anaamini wachezaji wa Yanga watapambana kuhakikisha wanamaliza msimu kwa kupata kikombe hicho cha ubingwa wa Bara.


"Ligi ni ngumu na ina ushindani, hakuna mechi rahisi kwa sababu kila timu inajiandaa kusaka ushindi," alisema mchezaji huyo.

Mganda huyo Jumamosi alitoa pasi iliyozaa bao la tatu lililofungwa na Hussein Javu katika ushindi wa 3-o walioupata Yanga kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mkoani Tabora dhidi ya Rhino Rangers.

Baada ya kurejea kutoka mkoani Tabora juzi usiku, Yanga iliingia kambini jana jioni katika makao makuu ya Klabu yao yaliyopo mtaa wa Twiga Jangwani kujiandaa na mechi ya kesho dhidi ya Prisons kutoka ya Mbeya.

Okwi atakumbukwa na mashabiki wa Simba kutokana na kuifungia timu hiyo na kuonyesha kiwango cha juu wakati ilipoibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Yanga.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC