Ruka hadi kwenye maudhui makuu

HANSPOPE AZIFANYIA UMAFIA AZAM, YANGA, AMREJESHA KAPOMBE MSIMBAZI

KIUNGO anayeweza kucheza nafasi za ulinzi pia, Shomary Kapombe atarejea kwenye kikosi cha Simba SC msimu ujao baada ya makubaliano yaliyofikiwa baina ya klabu hiyo na AS Cannes ya Ufaransa.

Habari za ndani kutoka Simba SC ambazo tumezipata, zinasema kwamba Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amefikia makubaliano mazuri na AS Cannes juu ya Kapombe.

“Pope amezungumza na Cannes na wamekubaliana kulipana fedha ili Kapombe arejee Simba SC,” kimesema chanzo kutoka Simba SC na alipotafutwa Poppe mwenyewe alisema; “Nipo safarini, lakini kwa kifupi Kapombe anarudi Simba SC kwa Mkataba wa miaka mitatu kuanzia msimu ujao,”alisema.
  
Pope amesema kwamba Simba SC imekubali kuilipa Cannes Euro 33,000 ambazo sawa na Sh. Milioni 66 ili kurejeshewa mchezaji wake huyo.

Kapombe alitolewa bure kwenda AS Cannes katikati ya mwaka jana akiwa bado ana Mkataba na klabu hiyo ya Msimbazi, unaomalizika Aprili mwaka huu.

Baada ya kuwa Ufaransa kwa zaidi ya miezi mitatu, Kapombe alirejea nchini Novemba mwaka jana kwa ruhusa maalum ya kuja kuichezea timu ya taifa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe.

Baada ya mchezo huo, mchezaji huyo akaamua kubaki moja kwa moja nyumbani akidai halipwi mishahara.

Kapombe mwenyewe amekuwa mgumu kuzungumzia suala hilo, lakini tayari kuna habari kwamba Yanga SC na Azam zinamtaka mchezaji huyo.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC