Ruka hadi kwenye maudhui makuu

BARCELONA YAITOA MASHINDANONI MAN CITY

Manchester City baada ya mechi yao na Barcelona
Dani Alves alifunga bao dakika za mwisho ya mechi yao na kuipa Barcelona ushindi dhidi ya Manchester City na kufuzu kwa robo fainali ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya.

Manchester ambayo ilinyukwa magoli mawili kwa bila katika mechi ya raundi ya kwanza, ilipoteza nafasi nyingi wakati wa mechi hiyo nzuri zaidi ikiwa ni mkwaju wa Samir Nasri uliookolewa na kipa wa Barcelona Victor Valdes.

Lionel Messi alikamilisha pasi ya Cesc Fabregas kati kati mwa kipindi cha pili kabla ya Pablo Zabaleta kuonyeshwa kadi nyekundu.


Baada ya kushinda kombe la Ligi mwishoni mwa Juma lililopita na kupoteza mechi ya robo fainali ya kuwania kombe la FA dhidi ya Wigan, vijana hao wa Manuel Pelegrini sasa wamesalia la katika kinyanganyiro cha kuwania kombe la Ligi Kuu ya Premier na kwa sasa inashikilia nafasi ya nne ikiwa alama tisa nyuma ya vinara wa sasa Chelsea lakini ingali na mechi tatu mkononi.

Manchester City sasa itasubiri kwa hamu kuu habari kuhusu jeraha lililomlazimisha Sergio Aguero, ambaye tayari amekosa mechi kadhaa msimu huu, kuondolewa baada ya kipindi cha kwanza.

Hata hivyo City waligadhabisha na uamuzi wa refa wa mechi hiyo kutoka Ufaransa Stephan Lannoy, wa kupuuza kile kilichoonekana kuwa penalti ya wazi baada ya Gerard Pique kumfanyia madhambi Zabaleta ambaye alipewa kadi nyekundu baada ya kuonyesha kadi ya njano ya pili.

Machester City ilipata bao lake la kuvutia machozi kupitia kwa nyota wake Jeleon Lescott.
Barcelona imefuzu kwa robo fainali kwa jumla ya magoli manne kwa m

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC