Ruka hadi kwenye maudhui makuu

BAO LA LALA SALAMA LAIBEBA SPURS

Christian Eriksen

Gylfi Sigurdsson alifunga bao la ushindi dakika ya mwisho baada ya Christian Eriksen kufunga mawili na kusaidia Tottenham Hotspur kujikwamua kutoka 2-0 chini na kulaza Southampton 3-2 katika Ligi ya Premia Jumapili.
Sigurdsson alifunga bao kutoka kwa kiki ya raia wa Denmark Eriksen na kuweka hai matumaini ya Spurs ya kumaliza katika nne bora. Wamo nambari tano na alama 56, sita nyuma ya Arsenal walio wa nne wakiwa wamecheza mechi moja zaidi.

“Lazima utafute njia ya kushinda, haukuwa mteremko, haukuwa uchezaji wa kupendeza lakini mwishowe lazima utafute njia ya kushinda,” meneja wa Spurs Tim Sherwood aliambia wanahabari.

“Tumejikwamua na baada ya mechi mbili au tatu za vichapo, tumeonyesha ustadi wetu na hilo ndilo natafuta.”

Southampton walitawala mechi mwanzoni wakiwa na soka safi ya nipe nikupe na makosa mawili kutoka kwa beki wa kulia wa Spurs Kyle Naughton yaliwezesha wageni hao kuwa mbele 2-0 baada ya dakika 28
.

Jay Rodriguez aliangukia mpira eneo la hatari baada ya Naughton kukosa kuupata vyema mpira uliokuwa umeondolewa na kipa Artur Boruc, na kuwezesha Rodriguez kupata fursa ya kuteka macho ya meneja wa Uingereza Roy Hodgson.

Rodriguez, mmoja wa wachezaji wa Saints anayesaka nafasi katika kikosi cha Kombe la Dunia cha Hodgson alimbwaga kipa wa Spurs Hugo Lloris na kufunga bao lake la 15 msimu huu baada ya dakika 19.
Saints waliongez ala pili baada ya Naughton kufanya kosa tena na kukosa kuondoa mpira vyema jambo lililomuwezesha Adam Lallana mwishowe kumbwaga Lloris na kufunga la pili.

Kosa jingine, wakati huu kutoka kwa beki wa kulia Nathaniel Clyne, liliwezesha Spurs kurejea tena kwenye mechi dakika nne baadaye aliporuhusu krosi kutoka kwa Naughton ipite chini ya miguu yake na kufikia Eriksen aliyefunga kutoka karibu sana na goli.

Dakika moja baada ya kipindi cha pili kuanza, Spurs walisawazisha baada ya Roberto Soldado kumzidi nguvu difenda Dejan Lovren na kutoa krosi kwa Eriksen ambaye alifunga tena.

Sigurdsson, aliyeingia kama nguvu mpya baada ya mapumziko kuchukua nafasi ya Moussa Dembele, alikamilisha ushindi kwa kombora la chini dakika za mwisho.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa