BAADA YA KUSOTA, BATAROKOTA AULA TUZO ZA KILL MUSIC AWARD


HATIMAYE mwanamuziki  Batarokota amefanikiwa kuingia kwenye tuzo za muziki za Kilimanjaro Music Award mwaka 2014, kwa mujibu wa waandaaji wa tuzo hizo, Batarokota ameingia na wimbo wake Kwejaga nyangisha.

Tayari makundi ya washiriki wa tuzo hizo yameshapangwa hukua akichuana na wanamuziki wengine wenye majina makubwa hapa nchini, makundi hayo yanahusisha wanamuziki maarufu kama Diamond lakini kundi la Batarokota lipo kama ifuatavyo.

Wimbo bora wenye vionjo vya asili ya Kitanzania
1 Kwejaga nyangisha-Batarokota
2 Nalonji-Kumpeneka
3 Bora Mchawi-Dar Bongo massive
4 Tumbo lamsokota-Ashimba
5 Aliponji -Wanakijiji
6 Agwemwana-Cocodo African music band

Batarokota amekuwa katikamafanikio mazuri baada ya kutengenezxa wimbo huo kupitia njia ya video, hivi karibuni alifanya ziara yake ya kimuziki katika nchi za Swaziland na Afrika Kusini.