Ruka hadi kwenye maudhui makuu

UHURU SELEMAN AINYIMA UBINGWA SIMBA

Uhuru Suleiman amesema timu yake ya Simba ina mazingira magumu ya kutwaa ubingwa kutokana na ushindani mkali iliopo kwenye ligi kuu ya Bara  ugumu uliopo katika duru la pili.

Lakini, kiungo huyo amesema, Simba bado ina nafasi ya kutwaa taji hilo kama itarekebisha makosa yaliyojitokeza nyuma na kufanya vizuri katika mechi zilizosalia.

Akizungumza na Nipashe katikati ya wiki, Uhuru ambaye hakuambatana na Simba jijini Mbeya ambako ilitoka sare ya 1-1 na Mbeya City Jumamosi iliyopita alisema ligi imekuwa gumu kutokana na timu kukamiana na ndiyo maana timu yake haifanyi vema.

"Ligi katika duru la pili imekuwa ngumu mno," alisema Uhuru nyota wa zamani wa Mtibwa Sugar na Coastal Union.


"Timu zinakamia na zinafukuzia pointi tatu."

Hata hivyo alisema pamoja na Simba kuonekana kuyumba katika mechi zake za karibuni, bado ina nafasi ya kuwa bingwa kwa sababu kuna mechi nyingi kabla ya msimu kufungwa.

Simba iliyopoteza pointi saba katika mechi zake tatu zilizopita kwa kupata sare mbili dhidi ya Mtibwa Sugar na Mbeya City na kulala kwa Mgambo JKT ipo nafasi ya nne kwenye msimamo, ikiwa pointi nne nyuma ya viongozi Azam wenye mechi mbili mkononi juu.

Mabingwa hao wa zamani kesho wataikabili JKT Ruvu iliyo katika nafasi za katikati za msimamo na ambayo mwalimu wake mpya kocha msaidizi wa zamani wa Yanga, Fred Felix 'Minziro' alipokelewa na kipigo cha 6-0 kutoka kwa Prisons katikati ya wiki.
 

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa