
Msanii kutoka marekani anayefahamika kwa jina la Elijah King, juzi aliibuka mshindi kwa kunyakua tuzo ya Super Song iliyoandaliwa na shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA.
Nyimbo iliyompa ushindi mwanamuziki huyo ni nyimbo ya VIDA, Nyimbo ambayo mashairi yake yamesimama na ya kuvutia kiasi kwamba ikazifunika nyimbo nyingine zote zilizokuwa zinashindania tuzo hiyo.
Kutokana na ubora wa nyimbo hiyo iliwaweka majaji hao katika wakati mgumu kuchuja na nyimbo nyingine, Na kuzidi kuipa nafasi nyimbo hiyo kwa kura nyingi hatimaye juzi kuibuka mshndi wa nyimbo bora ya FIFA 2014 WORLD CUP SUPER SONG COMPETETION.
Mashindano hayo ambayo juzi yalikuwa fainali ambapo staa Ricky Martin, alipomtangaza rasmi Mmarekani huyo kuwa ni mwanamuziki bora wa FIFA mwaka 2014.Na wimbo wake kuwa ni wimbo bora katika mashindano hayo.
Kutokana na tuzo hiyo FIFA imempa shavu mwanamuziki huyo ya kufanya kazi na maprodyuza machachari wa Super Song, ambao ndio hao waliouandaa wimbo huo bora wa FIFA.pamoja na kufanya kazi na Global Super star anayefahamika kwa jina la Ricky Martin.

Elijah King alifurahi sana na kuishukuru FIFA juu ya mashindano hyo waliyoyaandaa, maana imeleta changamoto kubwa katika maendeleo ya kazi zake na kumfanya azidi kuwa kinara na kutambulika dunia nzima.
Si jambo la kushangaza mmarekani huyo kupata tuzo hiyo,hususani katika ulimwengu huu wa sasa wamarekani ndiyo wanaoongoza na kuwa kinara katika tasnia ya muziki.

Wanamuziki wakubwa kama Rihana n.k nao pia walikuwa wanaigombea tuzo hiyo, lakini mwisho wa siku staa huyo kuibuka kidedea. Na kuwaacha nyota hao na mshangao.
Hivyo basi michuano hiyo ikianza tutazidi kuusikia wimbo huo bora unafahamika kwa jina la vida.