Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MASIKINI EMMANUEL OKWI! TFF YAMKANDAMIZA TENA KWENYE SAKATA JINGINE,IKIBAINIKA KUFUNGIWA MAISHA.

Sakata la uhamisho wa mshambuliaji Emmanuel Okwi limeanza kuwatafuna vigogo wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakidai kushughulikia suala hilo kiushabiki badala ya kufuata taratibu.

Taarifa ya Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura jana ilisema kuwa kiongozi wa idara ya Takwimu, Sabri Mtulla analalamikiwa na  shirikisho hilo kwa madai ya kuidanganya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kuwa hakukuwa na pingamizi  dhidi ya  usajili wa Okwi huku akijua wazi kuwa jambo hilo si kweli.

“Kamati ilikutana mara ya kwanza, ikahoji kama kuna pingamizi lolote dhidi ya Okwi, lakini Mtulla alidanganya kuwa hakuna, kamati ilivyokutana kwa mara ya pili ikabaini pingamizi lilikuwepo, ila kiongozi huyo alificha wakati alijua wazi kuwa Simba walikuwa wameweka pingamizi  wakipinga Okwi kusajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.


“Kwa mujibu wa kanuni, malalamiko hayo yamefikishwa kwenye Kamati ya Maadili ambayo itachunguza ili kujiridhisha kama yana msingi au la. Ikibaini kuwa kuna kesi ndipo walalamikiwa watafika mbele ya kamati hiyo kujibu mashtaka yao.”

Hata hivyo mtandao huu ulipomtafuta Mtulla kuhusiana na suala hilo alisema kwa kifupi: “Ofisi ndiyo inayonituhumu nimefanya udanganyifu, mimi nasubiri niitwe nitoe utetezi wangu, ili suala nalijua undani wake kuanzia mwanzo hadi lilipofika sasa, nitaweka wazi kila kitu, kwa kifupi wamelikoroga sasa wanatafuta pa kuangushia jumba bovu.”

Sinema ya usajili wa mshambuliaji huyo raia wa Uganda ilianza   Mei 19, 2013 wakati Shirikisho la Soka nchini Uganda (Fufa) kupitia mtendaji wao mkuu, Edgar Watson lilipotuma barua kwa Shirikisho la soka  la Tunisia likimwombea kibali  Okwi kujiunga na kambi ya timu ya taifa (Uganda Cranes) iliyokuwa inajiandaa na michezo miwili dhidi ya Angola na Liberia  kufuzu kushiriki Kombe la Dunia  mwaka  huu nchini Brazil.

 Michezo hiyo ilikuwa ichezwe  Juni 8 na 15 jijini Kampala na baada ya michezo hiyo Okwi hakurejea  klabuni kwake, Etoile du Sahel.

Simba SC iliyomuuza kwa Etoile ilitaka kumrejesha kundini mwaka jana, lakini aliikwepa na  kwenda  SC Villa ya Uganda ili apate nafasi ya kucheza fainali za  wachezaji wa ligi za ndani (Chan).

Okwi aliuzwa na Simba kwa Etoile kwa ada ya Dola 300,000 lakini Watunisia hao walishindwa kuwalipa Simba fedha za usajili  huo kwa wakati, pia Okwi aligoma kuwachezea Waarabu hao  kwa madai ya kushindwa kuheshimu makubaliano ya  kimkataba.

Baada ya mgomo uliochukua miezi kadhaa SC Villa ambayo ndiyo iliyomkuza Okwi kabla ya kumuuza Simba, iliomba Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kumruhusu arudi Uganda ili asipoteze kiwango chake na Fifa ilimruhusu kwa kumpa kibali cha miezi sita wakati suala lake likitatuliwa.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC