Jeshi la Polisi limewatawanya wafuasi wa Katibu Mkuu wa CHADEMA aliyevuliwa wadhifa Zitto Kabwe na wafuasi watiifu kwa chama hicho waliotaka kupigana baada ya Mahakama Kuu kuhairisha kutoa maamuzi ya kesi iliyofunguliwa na Zitto dhidi ya chama chake.
Kutokana na vurugu hizo sasa hali ya hewa ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini imeanza kuwa mbaya, jana chama hicho kilitangaza kuwavua uanachama waliokuwa makada wa chama hicho Samosn Mwigamba na Kitila Mkumbo kilichodaiwa kutaka kukisaliti chama hicho.
Zito Kabwe ambaye alivuliwa nyadhifa zake zote ndani ya chama hicho alipeleka shauri lake mahakamani la kutaka asivuliwe uanachama ambapo leo hii mahakama ilitangaza kuahirisha kesi hiyo ambapo mapambano kati ya wafuasi wa mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini na wale wa chama hicho ambao ni watiifu.
Kupelekea vurugu hizo jeshi la polisi lilifanikiwa kuwatawanya wafuasi hao na kuzima jaribio lao la kupambana katika eneo hilo maalum kwa usuruhishi wa kisheria, Chadema imejikuta ikizozana wao kwa wao na huenda ikapelekea kukiathili chama hicho katika uchaguzi mkuu wa nchi mwakani.