Ruka hadi kwenye maudhui makuu

BODI YA LIGI YAIKABA KOO YANGA KUHUSU AZAMTV

Uongozi wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), umesema Yanga itake isitake AzamTV itarusha mechi zote na kama hawataki ni bora wakajitoa kwenye Ligi.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Ahmad Yahaya akijibu azimio lililofikiwa na viongozi na wanachama wa Yanga wa kugomea AzamTV kuonyesha mechi zake.

Yahaya alisema Yanga hawana haki ya Televisheni za Ligi Kuu mwenye haki hizo ni Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).


“Haki za Televisheni za Yanga wanazo wenyewe wala sisi hatujawaingilia, wana uamuzi wao kama watauza haki hizo kwenye mechi zao za kirafiki, mechi za kimataifa hilo ni jukumu lao wala sisi halituhusu.

“Lakini haki za Ligi Kuu ni za TFF,  Ligi Kuu ni mali ya TFF ambayo Bodi inasimamia, na Yanga itaheshimu misingi, kanuni, na maelekezo yote yanayotolewa na TFF, Azam imeingia mkataba na TFF kupitia Bodi ya Ligi ambao ndio wasimamizi, Yanga hawana haki yoyote ya kukataa mechi zao zisionyeshwe na AzamTV.

“Wao Yanga kama hawataki AzamTV iwatangaze basi ijitoe kwenye ligi sisi hatutawatangaza, lakini madhali wapo kwenye ligi basi mechi zao zitaonyeshwa na huo ni msimamo wa Bodi na Serikali,” alisisitiza

Yahaya alisema kuwa fedha za Yanga Sh75 milioni ambazo wamezisusa bado zipo kwenye akaunti ya Ligi Kuu na iwapo muda wowote wakiziitaji watapatiwa fedha hizo.

Kauli ya Yahaya imekuja siku chache baada ya Yanga kuzungumzia suala la mkataba wa AzamTV kwenye mkutano wao mkuu na wanachama kuwataka viongozi wao kuwapeleka mahakamani Azam kwa kukiuka agizo la Yanga la kutaa mechi zao za Ligi kuonyeshwa live na kampuni hiyo.

Mwenyekiti wa Yanga, Yusufu Manji alitoa mchanganuo wa udhamini huo kwa kusema “Azam wanataka kuonyesha mechi zetu kwa Sh100 milioni, kwa mechi 26 tunazocheza ligi nzima hiyo ni sawa na Sh3 milioni kwa kila mechi, kwa mechi yetu moja tunapata zaidi ya Sh3 milioni na ile inayotukutanisha na Simba tunaingiza zaidi ya Sh100 milioni na kuhoji wanachama wake udhamini huo ni halali au siyo halali ambapo kwa pamoja waliukataa kwa kile walichoeleza siyo halali na kutaka Azam wapelekwe mahakamani.

Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Clement Sanga akizungumzia suala hilo mara baada ya mkutano huo alisema, “Kuna kampuni ambayo tumeingia nayo mkataba SGM ya Kenya kwa ajili ya kuonyesha mechi yetu ya raundi ya kwanza dhidi ya Al Ahly ya Misri, kampuni hii kwa mechi moja tu inatupa Dola 55,000 (sawa na Sh90 milioni).

“Tulikubaliana na Azam TV  wao wabaki na kipindi cha Yanga Soccer Show, sisi tuendelee na Haki zetu za Televisheni na Zuku, lakini yaliyotokea hapa katikati yanajulikana,” alisema.

“Wanachama wameamua tuwapeleke mahakamani AzamTV, lakini sisi kama viongozi tutakaa na uongozi mpya wa TFF, na wanasheria wetu kuangalia upya suala hili, milango bado ipo wazi kwa Azam kukaa meza moja na sisi.”alisema Sanga.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC