Ruka hadi kwenye maudhui makuu

PELLEGRINI SASA AIGEUKIA ARSENAL.

Manuel Pellegrini wa Manchester City amekiri kwamba hatua yake ya kuweka freshi wachezaji wake kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya viongozi Arsenal Jumamosi ilisaidia kwenye ushindi wao wa kushangaza wa 3-2 wakiwa Bayern Munich.

Usiku huo wa kihistoria kwa klabu hiyo, City walipambana kutoka mabao mawili chini na kufikisha kikomo mkimbio wa ushindi wa mechi 10 mfululizo za Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya wa mabingwa hao huku kocha wa Bayern Pep Guardiola akikabidhiwa kichapo chake cha kwanza katika dimba kuu akiwa na timu hiyo ya Ujerumani.

Bayern pia walishindwa mara ya kwanza nyumbani – baada ya kushinda mara 18 Munich – tangu washindwe na Arsenal 2-0 wakiwa nyumbani mikononi mwa Arsenal wakati wa awamu ya muondoano ya msimu uliopita katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwezi Machi.


Huku timu zote mbili zikiwa tayari zimefuzu kwa awamu ya muondoano, City walilipiza kichapo cha 3-1 mwezi Oktoba walichokabidhiwa na Bayern uwanjani Etihad , lakini bado walimaliza wa pili nyuma ya Wajerumani hao katika Kundi D, timu zote mbili zikiwa na alama 15.

Winga wa City James Milner alikamilisha kujikwamua kwao kwa bao la dakika ya 62, ingawa ushindi wa 4-2 ungepelekea vijana hao wa Pellegrini kusonga wakiwa washindi wa Kundi D.

Pellegrini aliingiza straika wa Uhispania Alvaro Negredo na kuondoa David Silva, aliyerudi kutoka kwa jeraha la misuli ya chini ya mguu, kucheza dakika 20 za mwisho, lakini Mchile huyo alikiri kwamba alikuwa akifikiria kuhusu Gunners sawa na alivyokuwa akifikiria kuhusu bao la nne.

"Ilikuwa ni muhimu kwetu kupata bao la nne, lakini ingekuwa ni kuhatarisha zaidi kuendelea kuchezesha David Silva," alisema kocha huyo wa City.

“Ilikuwa ni muhimu kwetu kuongoza kundi, lakini tuna mechi kali sana Jumamosi na hilo halikuwa jambo la muhimu zaidi.”

Jambo la kushangaza ni kwamba, City walifanikisha ushindi huo wao muhimu Ulaya hata baada ya mafowadi nambari wani Sergio Aguero na Negredo, pamoja na nahodha Vincent Kompany kuanza wakiwa kwenye benchi.

“Ulikuwa ni ushindi muhimu kwa klabu, sio tu kwangu pekee,” akasema Pellegrini ambaye awamu alisema kwenye televisheni kwamba hakuwa anajua kwamba ushindi wa 4-2 ungepelekea timu yake kumaliza ikiwa ya kwanza kwenye kundi.

“Ujumbe wa kwanza kwa kikosi ni kwamba wanaweza kushinda bila akina Kompany, Aguero na Negredo.”

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC