Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MWALUSAKO AKUMBWA NA KIMBUNGA JANGWANI, NJOVU AMRITHI.

Uongozi wa Yanga umemtambulisha Beno Njovu kuwa Katibu Mkuu mpya wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Lawrence Mwalusako aliyekuwa akiikaimu kwa mwaka mmoja baada ya Celestine Mwesigwa kufukuzwa Septemba mwaka jana.

Kamati ya Utendaji ya Yanga, ilimtambulisha rasmi Njovu ambaye wameingia naye mkataba wa mwaka mmoja, mbele ya waandishi wa habari, wajumbe wa Baraza la Wazee la Yanga na Baraza la Wenyeviti wa Matawi wa klabu hiyo kwenye makao makuu ya Yanga jijini Dar es Salaam jana.

Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto alisema, Njovu alianza kuitumikia nafasi hiyo kuanzia jana na Mwalusako atakuwa naye kwa kipindi cha mwezi mmoja mpaka atakapokabidhi kazi rasmi Januari mwakani.


Akizungumza mara tu baada ya kutambulishwa rasmi, Njovu aliahidi kuitumikia klabu hiyo kwa uaminifu na uadilifu akifuata maagizo ya Kamati ya Utendaji na miiko ya klabu hiyo.

"Naushukuru uongozi wa Yanga kwa kutambua umuhimu wangu na kuamua kunikabidhi jukumu hili. Naamini uzoefu wangu katika masuala ya utawala na biashara utasaidia katika kuiendeleza klabu," alisema Njovu, ambaye kitaaluma ana Shahada ya Pili (Uzamili) katika Utawala wa Biashara (Masters in Business Adminstration).

Baada ya timu kuanza vibaya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita ikitoka suluhu dhidi ya Prisons jijini Mbeya Septemba 15, mwaka jana kabla ya kupokea kichapo kikali cha mabao 3-0 dhidi ya mabingwa wa Tanzania Bara 1999 na 2000, Mtibwa Sugar mjini Morogoro Septemba 19, mwaka jana, uongozi wa Yanga uliamua kumtimua aliyekuwa kocha wao, Mbelgiji Tom Saintfiet na mikoba yake kuchukuliwa na Mholanzi Ernie Brandts.

Uongozi wa mabingwa hao wa Tanzania Bara, uliamua kuwafungashia virago pia Mwesigwa na aliyekuwa Ofisa Habari wao, Louis Sendeu na nafasi yake kuchukuliwa na Kizuguto.

Wakati huo huo, uongozi wa Yanga umesema mkutano mkuu wa wanachama utafanyika Januari 19, mwakani huku ukiweka wazi kwamba uchaguzi mkuu wa klabu hiyo utafanyika wiki mbili baada ya msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Soka nchini (TFF), ligi hiyo iliyoanza Agosti 24, mwaka huu, itamalizika Jumapili Aprili 27, mwakani, hivyo uchaguzi mkuu wa Klabu ya Yanga utafanyika katikati ya mwezi Mei mwakani.

Ofisa Habari wa Yanga (Kizuguto) alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa baada ya kukutana na viongozi wa Matawi ya Yanga, uongozi uliopo madarakani umeomba uchaguzi mkuu wa klabu hiyo ufanyike wiki mbili baada ya ligi kuu kumalizika badala ya Juni mwakani kwa mujibu wa Katiba ya Yanga.

"Mwenyekiti ametangaza rasmi kutogombea tena uenyekiti na nafasi yote katika uchanguzi mkuu ujao na atabaki kuwa mwanachama na shabiki wa Klabu ya Yanga. Hili ameliamua mwenyewe binafsi bila shinikizo na kikubwa amefuata demokrasia," alisema Kizuguto.

Uongozi ambao uko madarakani Yanga ulikuwa ukimalizia kipindi cha miaka miwili iliyokuwa imebaki katika utawala wa miaka minne wa aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Wakili Lloyd Nchunga aliyejiuzulu Mei 24, mwaka jana.

Kizuguto alisema uongozi uliopo madarakani una miezi saba kabla ya uchaguzi mkuu mwakani, hivyo kwa sasa unajitahidi kukamilisha shughuli zote ambazo ulianza kuzifanya ndani ya Yanga.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC