Ruka hadi kwenye maudhui makuu

JAKAYA KIKWETE KAMA OBAMA 'SAUZI' KUMUAGA ,MANDELA.

Serikali ya Afrika Kusini, imetoa orodha ya majina ya wakuu wa nchi na Serikali 91 ambao wamethibitisha kushiriki katika shughuli zinazohusiana na safari ya mwisho ya Rais wa kwanza mzalendo wa taifa hilo, Nelson Mandela.

Jina la Rais Jakaya Kikwete ni la kwanza katika orodha hiyo inayowaweka viongozi hao katika makundi kutokana na mabara wanakotoka. Rais Kikwete alitarajiwa kuwasili jana usiku tayari kuhudhuria Ibada ya Kitaifa ya Mandela ambayo imepangwa kufanyika leo kwenye Uwanja wa FNB (Soccer City).

Kabla ya Serikali kutoa orodha hiyo, Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Maite Nkoana-Mashabane alisema wakuu wa nchi na Serikali 53 walikuwa wamethibitisha lakini jana mchana idadi hiyo ilikuwa imeongezeka na kufikia 91. Kulikuwa na wasiwasi kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka na kuzidi 100.

Msemaji wa Wizara ya Uhusiano wa Kimataifa ya Afrika Kusini, Clayson Monyela aliwataja marais wengine kutoka Afrika kuwa ni kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Joseph Kabila, Hifikepunye Pohamba wa Namibia, Mike Sall wa Senegal, Allessane Ouattara wa Cote d’Ivoire, Goodluck Jonathan wa Nigeria, Robert Mugabe wa Zimbabwe, Dennis Sassou-Nguesso wa Congo Brazaville, John Dramani wa Ghana na Ali Bongo wa Gabon.


Kutoka Amerika ya Kusini ni marais Nicolus Maduro Moros wa Venezuela na Dilma Rousseff wa Brazil ambaye ataambatana na marais wanne wastaafu wa nchini kwake.

Waziri Mkuu wa Bahamas, Perry Christie, Rais wa Guyana, Donad Ramotar, Rais wa Haiti, Michael Martelly na Rais wa Jamaica, Portia Miller, wakati kutoka Asia, kutakuwa na marais Pranab Mukherjee wa India na Hamid Karzai wa Afghanistan.

Rais Francois Hollande wa Ufaransa, Waziri Mkuu wa Australia, Tony Abbot, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon

Tayari Rais wa Marekani, Barrack Obama na mkewe Michelle walishathibitisha kushiriki, pia watangulizi wake, Bill Clinton, George W. Bush na Jimmy Carter wanatarajiwa kushiriki katika mazishi ya Mandela yatakayofanyika Qunu, Mthatha Jumapili.

Armando Guebuza wa Msumbiji, , Abdelkader Bensalah wa Algeria, Makamu wa Rais wa Angola, Manuel Vicente, Rais wa Niger, Issoufou Mahamdou, Kaimu Rais wa Agentina, Amado Boudou, Waziri Mkuu wa New Zealand, John Key na Rais wa Bangladesh, Abdul Hamid MD Abdul.

Malkia Haakon wa Norway, Mfalme wa Philippe wa Ubelgiji, Rais wa Pakistan, Mamnoon Hussain, Rais wa Benin, Boni Yayi, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas, Rais wa Botswana, Seretse Ian Khama, Rais wa Ureno, Anibal Cavaco Silva na Mfalme wa Saudi Arabia, Muqrin bin Abdulaziz Al-Saud, Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, Rais wa Saharawi, Mohamed Abdelaziz, Waziri Mkuu wa Canada,

Stephen Harper wa Chad, Idriss Deby Itno, Rais wa Serbia, Tomislav Nikolic, Makamu Rais wa China, Yuanchao, Rais wa Shelisheli, James Alix Michel, Rais wa Comores, Dr Ikiliou Dhoinine na Mfalme wa Hispania, Felipe de Borbon.

Rais wa Sri Lanka, Mahinda Rajapaksa, Makamu Rais wa Sudan, Hassan Salih, Rais wa Suriname, Desire Delano Bouterse, Rais wa Slovenia, Pahor, Rais wa Croatia, Josipovic Ivo, Rais wa Sudan Kusini, Salva Kir Mayardit, Rais wa Cuba, Raul Castro Ruz, Rais wa Djibouti, Ismail Omar Guelleh, Waziri Mkuu wa Swaziland, Dr Sibusiso Dlamini, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Ato Hailemariam Dessalegn na Rais wa Equatorial Guinea, Obiang Mbasogo.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC