Ruka hadi kwenye maudhui makuu

IVO MAPUNDA AMWAGA WINO RASMI SIMBA MIAKA MIWILI.

KIPA namba moja wa Tanzania, Ivo Philip Mapunda, jana usiku amesaini Mkataba wa mwaka mmoja na nusu kujiunga na klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam, akitokea Gor Mahia ya Kenya.

Ivo anasaini Simba SC, baada ya kung’ara akiwa na kikosi cha Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mwaka huu.

Ivo aliiongoza Kilimanjaro Stars kufika Nusu Fainali ya Challenge baada ya kuwatoa waliokuwa mabingwa watetezi Uganda ‘The Cranes’ kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90, kipa huyo akicheza mikwaju miwili.

Akizungumza baada ya kusaini Simba SC, Ivo alisema kwamba ameamua kusaini timu hiyo Mtaa wa Msimbazi baada ya kuridhishwa na maslahi aliyopewa.

   
“Sina wasiwasi, mimi ni kipa mzoefu na hata Watanzania wanajua uwezo wangu, baada ya kusaini, sasa ni kazi tu, kikubwa naomba ushirikiano na benchi la Ufundi, uongozi, wachezaji wenzangu na mashabiki na wadau kwa ujumla, ”alisema Ivo aliyewahi kudakia Yanga SC.

Ivo Philip Mapunda alizaliwa Novemba 14, mwaka 1979 na kisoka aliibukia katika klabu ya Tukuyu Stars kabla ya kuhama Prisons zote za Mbeya, baadaye Moro United mwaka 2005 kabla ya kutua Yanga msimu uliofuata, 2006.

Aliidakia Yanga hadi 2009 akahamia St George ya Ethiopia alikopiga kazi msimu mmoja, akarejea nyumbani kuidakia African Lyon 2011 kabla ya 2012 kuhamia Bandari ya Mombasa, Kenya ambako alifanya kazi kwa miezi sita akasajiliwa na Gor Mahia.

Ivo anamaliza Mkataba wake Gor Mahia Desemba 16, mwaka huu na ataidakia kwa mara ya mwisho klabu hiyo katika mechi ya Kombe la DSTV Desemba 14 dhidi ya Tusker FC na baada ya hapo atapakia kila kilicho chake na kuja kuanza maisha mapya Msimbazi. 

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC