Nicklas Bendtner anatumai kuwa bao lake alilofungia viongozi wa Ligi ya Premia Arsenal dhidi ya Hull Jumatano litapelekea yeye kurejea tena katika kikosi cha kwanza.
Raia huyo wa Denmark, ambaye aliitwa tena na meneja Arsene Wenger ili kupumzisha straika Olivier Giroud, alifunga bao la na kuweka wenyeji hao kifua mbele dakika ya pili – bao la kwanza la Bendtner kufungia Arsenal tangu Machi Machi 2011.
Arsenal walishinda 2-0 kwenye mechi hiyo iliyochezewa Emirates Stadium na wanaendelea kubaki alama nne mbele kwenye kilele cha jedwali.
Bendtner alikuwa amekabiliwa na hali isiyotabirika Arsenal baada ya kukopeshwa kwa klabu nyingine na kasha akagonga vichwa vya habari mwezi uliopita baada ya kuonya na polisi kwa kuharibu jengo la nyumba ambayo yeye huishi.
"Nilihisi vizuri sana, ninafikiri kusherehekea kwangu kwa bao hilo kulionyesha hilo,” alisema Bendtner mwenye umri wa miaka 25 akiongea na Arsenal Player.
"Ilikuwa ndiyo mechi yangu ya kwanza ya Ligi Kuu msimu huu, na hivyo nina furaha sana kwamba nilifunga na kwamba tulishinda.
“Imekuwa vigumu kwa wachezaji ambao hawajakuwa kwenye timu kwa sababu tulikuwa katika hali nzuri sana na wachezaji ambao wamekuwa wakicheza wametamba.
"Kutokana na vile watu wanacheza kwa sasa, inaonekana ni kana kwamba kila anayeingia anafuata hilo, na hilo lilijionyesha tena kwa sababu kulifanywa mabadiliko kadha na kila mmoja alicheza vyema.”
Arsenal watakuwa wenyeji wa Everton Jumapili, na kisha wasafiri Napoli kwa mechi yao ya mwisho ya kundi katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kabla ya kukutana na Manchester City Jumamosi.
"Tunaisubiri sana kwa sababu tunajua hiki ni kipindi kigumu na tunahitaji kila mtu kuwa makini na macho sana, lakini tutakabili kila mechi wakati mmoja na kujaribu kuongeza alama kwenye jedwali,” alisema Bendtner.