Fowadi wa Swansea City Michu huenda akakaa nje hadi wiki nne baada ya kupata jeraha kwenye tindi ya mguu wake wakati wa kichapo cha 1-0 mikononi mwa Cardiff City, meneja Michael Laudrup alifichua Jumatano.
Mchezaji huyo wa umri wa miaka 27, aliyekuwa mfungaji bora wa mabao wa Swansea msimu uliopita akicheza nao mara ya kwanza, alilazimika kuondolewa uwanjani dakika ya 65 wakati wa kichapo hicho cha Jumapili wakiwa Cardiff katika Ligi ya Premia.
Alikuwa tayari ameondolewa kutoka kwa timu ya kucheza mechi ya Swansea Ligi ya Uropa dhidi ya Kuban Krasnodar Akhamisi lakini, akiongea kabla ya mechi hiyo itakayochezewa Urusi, Laudrup alisema jeraha hilo ni baya kuliko ilivyodhaniwa.
“Michu, mfungaji mabao bora wetu msimu uliopita, amekuwa akitatizika wiki chache zilizopita na hayuko sawa asilimia 100 na kwa bahati mbaya atakaa nje tena kwa wiki tatu au nne,” Ladrup aliambia kikao cha wanahabari, kwa mujibu wa nukuu katika vyombo vya habari vya Uingereza.
Laudrup alisema kuwa Michu, aliyechezea timu ya taifa ya Uhispania mara ya kwanza mwezi uliopita, atatumia kipindi hicho kupata matibabu kuhusu matatizo ya muda mrefu kwenye goti lake.
“Ninaposema kwamba hajakuwa sawa kabisa, ni kwa sababu amekuwa akitatizwa na magoti yake mawili kwa wiki nyingi, lakini alitaka tu kuendelea kucheza na yeye ni mmoja wa wachezaji wetu muhimu sana,” alisema raia huyo wa Denmark.
"Kwa hiivyo sasa kutokana na jeraha hili la tindi ya mguu, ni matumaini yetu kwamba magoti yake yataweza kutibiwa pia. Atakuwa Uhispania siku chache kudungwa sindano kadha.”