
Sasa imebainika kuwa mwenyekiti huyo wa Simba anatgumia kundi la mamluki ambao wengineo ni mashabiki wa kutupwa wa Yanga ambao hudiriki kuvaa jezi za Simba na kumuunga mkono, aidha ujanja huo umebainika na Simba wameandaa mpango rasmi wa kumng'oa Msimbazi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mjumbe mmoja wa kamati maalum ndani ta tawi moja maarufu jijini Dar es Salaam lkenye ushawishi mkubwa ndani ya klabu hiyo anasema kuwa ujanja wa Rage umejulikana hivi karibuni baada ya wapambe wake kuwakusanya mashabiki wa soka ambao wengine ni Yanga.
'Ni kweli Rage ametumia mashabiki wa soka na kujifanya wanampenda sana kisha kwenda uwanja wa ndege kumpokea, sisi wengine tunakaa nao na wengine ni marafiki zetu ambao tunawafahamu kama Yanga damu na wametuambia kuwa walialikwa na Rage ili kuwaonyesha Simba', alisema mumbe huyo.
A
