Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MWOMBEKI AREJEA KUIVAA YANGA KESHOKUTWA

Klabu ya soka ya Simba imepumua na kuwa na matumaini makubwa ya kumtumia mshambuliaji wake mrefu na mwenye nguvu, Betram Mombeki aliyekuwa akitajwa huenda asiwapo kwenye pambano lao la watani dhidi ya Yanga.


Mwombeki alitajwa kuwa katika hatihati ya kulikosa pambano hilo la watani wa jadi litakalochezwa kwenye Uwanja wa Taifa siku ya Jumapili baada ya kuumia mazoezini.

Hata hivyo, habari njema kwa wanachama na mashabiki wa Simba ni kwamba mshambuliaji huyo aliyesajiliwa na Simba akitokea Pamba ya Mwanza, amerejea tena uwanjani na kuna uwezekano mkubwa Jumapili atashirikiana na mfumani nyavu mahiri, Amisi Tambwe kuichachafya ngome ya Yanga.

Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga aliuambia mtandao huu jana kuwa, Mwombeki amerejea tena uwanjani baada ya hali yake kutengemaa na kuwapa matumaini makubwa ya kushuka dimbani Jumapili kuiangamiza Yanga.

Kamwaga alisema hata hivyo kikosi chao bado kitaendelea kukosa huduma za wachezaji wao nyota kama Henry Joseph, Issa Rashid 'Baba Ubaya' na Miraj Adam.

"Tunashukuru hofu ya kumkosa Mwombeki imeondoka baada ya mshambuliaji huyo kurejea tena dimbani, japo Simba itawakosa Henry Joseph ambaye hayupo kambini, Baba Ubaya, Miraj Adam na Abdallah Seseme ambao ni majeruhi," alisema Kamwaga.

Kamwaga alisema kikosi chao kina morali kubwa ya kushinda mechi ya Jumapili, licha ya kudai litakuwa pambano gumu.

Pia alisema katika kuwatia motisha wachezaji ili kuigaragaza Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, viongozi na 'matajiri' wa Simba wanatarajia kuteta na wachezaji kesho Jumamosi kwa lengo la kuwaweka sawa kisaikolojia pamoja na kuwapa nguvu zaidi ili kuwashinda Yanga.

"Viongozi na matajiri wa Simba wataitembelea kambi na kuzungumza na wachezaji kati ya Ijumaa (leo) na Jumamosi (kesho) ili kuwaweka sawa na kuhakikisha Yanga anakufa Jumapili Taifa," alisema Kamwaga.

Simba na Yanga zitakutana katika mchezo huo, huku Simba ikiwa na deni la kulipa kisasi cha kipigo walichopewa katika mechi yao ya mwisho ya ligi iliyopita iliyochezwa Mei mwaka huu ambapo Yanga ilishinda mabao 2-0.

Wakati Simba wakiwa na furaha hiyo, Yanga nao wamepata matumaini kufuatia kurejea kwa Ngasa, ambaye alikuwa akiuguma malaria.

Ngasa ambaye ametua Yanga akitokea Simba alikokuwa kwa mkopo, yuko katika kiwango cha juu hivi sasa akiwa amefunga magoli mawili na kutoa pasi za magoli mawili katika mechi zake tatu alizocheza tangu alipomaliza adhabu yake ya kufungiwa mechi sita za mwanzo wa msimu.

SIMBA WAJIBU MAPIGO


Kwa upande mwingine, uongozi wa Simba umesema hautishwi na tambo za watani wao wa jadi na umejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo huo utakaoanza saa 10:00 alasiri.

Mmoja wa viongozi 'wazito' wa Simba ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kuwa si msemaji wa klabu hiyo iliyoanzishwa 1936, alisema wamejipanga vizuri kuhakikisha wanaishangaza Yanga kwa kuishushia kipigo kikali Jumapili.

"Yanga wanaongea kujifurahisha. Katika mpira huwezi kusema unaingia uwanjani ukijua unashinda 3-0. Timu yetu imeandaliwa vizuri ili iibuke na ushindi dhidi yao," alisema kiongozi huyo huku akiweka wazi kuwa kikosi cha Simba kimeweka kambi yake Bamba Beach. Kigamboni jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mchezo huo.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC