Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KUUNGUA NYUMBA YA NIYONZIMA MKASA KAMILI HUU HAPA..........

Pigo jingine limeikumba klabu ya Yanga baada ya nyumba anayoishi kiungo wao wa kimataifa Mnyarwanda Haruna Niyonzima 'Fabregas' iliyopo Magomeni Makuti jijini Dar es Salaam kuungua moto jana na kusababisha hasara kubwa.


Niyonzima, ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha Yanga kinachonolewa na kocha Mholanzi Ernie Brandts, alikosa mazoezi ya timu hiyo jana kwenye uwanja wa shule ya sekondari Loyola uliopo Mabibo jijini Dar es Salam kufuatia tukio hilo.

Baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh alisema: "Niyonzima hajafika mazoezini kutokana na kuungua kwa nyumba anayoishi. Lakini taarifa zaidi anazo Kizuguto."

Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto alisema nyumba anayoishi kiungo huyo 'fundi' iliungua lakini hakuwa na taarifa za kina kuhusu balaa hilo.

Mwandishi alikwenda hadi nyumbani kwa Niyonzima ambako alimkuta nahodha huyo wa timu ya taifa ya Rwanda (Amavubi) akiwa amekaa nje ya nyumba hiyo huku uso wake ukionyesha kujawa na huzuni.

Niyonzima alisema moto umeunguza eneo la sebuleni la nyumba hiyo ambayo yeye ni mpangaji na kuteketeza vifaa vyote vilivyokuwapo zikiwamo skrini iliyokua imefungwa ukutani, redio (music system), makochi na samani nyingine za mamilioni ya shilingi.

"Ilikuwa saa inakaribia saa moja asubuhi nikiwa nimepumzika na familia yangu. Nikasikia mtu anatuamsha. Nilipofungua mlango, nikakutana na moshi mzito, sebuleni kwangu kulikuwa kunaungua," alisema Niyonzima.

Akizungumzia tukio hilo, Rabia Abeid, jirani wa Niyonzima, alisema aliona moshi mkubwa unafuka kutoka kwenye sebule ya nyota huyo tegemeo wa Yanga, hivyo kukimbia kwenda kuwaamsha.

Mke wa Niyonzima, Uwineza Naillah, alisema tukio hilo limeitia hasara kubwa familia yao na mmiliki wa nyumba hiyo kwa kuwa atalazimika kuweka madirisha mapya ya vioo na kufanyia ukarabati chumba huku wao wakilazimika kununua vifaa vipya vya sebuleni.

Niyonzima aliendelea kueleza kuwa baada ya kuona hali hiyo walipiga kelele ambazo zilijaza umati wa watu hasa majirani zao ambao walijitokeza kusaidia kuzima moto huo ambao pengine ungesababisha athari kubwa zaidi.

"Nyumba hii ina vyumba vitatu ninavyooishi mimi na familia yangu. Moto ulikuwa umetanda chumbani.

Majirani walijitokeza na kuanza kutusaidia kuzima moto huo kwa kuvunja madirisha ya vioo na kumwaga maji. Mpaka sasa hatujajua chanzo ni ni lakini tumeagiza fundi wa umeme aje aangalie kama moto huo umesababishwa na umeme," alisema Niyonzima.

"Nashukuru tulifanikiwa kuuzima moto lakini vitu vyote vilivyokuwa ndani hatukufanikiwa kuivitoa vikiwa salama. Akili yangu kwa sasa haiko sawa, sikumbuki thamani ya vitu vilivyokuwamo lakini haipungui Sh. milioni tano," alisema zaidi Niyonzima.

Kutokana na tukio hilo, Niyonzima alisema kuna uwezekano mkubwa wa kutoonekana uwanjani na huenda akakosa mechi ijayo dhidi ya mabingwa wa mwaka 1999 na 2000 wa Tanzania Bara, Mtibwa Sugar itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumapili.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alisema uongozi wa umezipokea kwa mashtuko taarifa za kuungua kwa nyumba anayoishi nyota wao na kwamba wanaangalia namna ya kumsaidia.

"Tutaangalia namna ya kumsaidia kutokana na tatizo hilo, lakini msaada wetu utakuwa siri yake na klabu ya Yanga," alisema Mwalusako.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Ngao ya Jamii sasa ni Simba na Yanga

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limebadilisha kanuni za mashindano za Ngao ya Jamii kutoka timu nne na sasa utaratibu utakuwa kama zamani. Bingwa wa Ligi Kuu bara atacheza na mshindi wa kombe la CRDB Cup "CRDB Federation Cup, na endapo kama bingwa wa ligi na CRDB atakuwa ni mmoja basi mshindi wa pili kwenye Ligi Kuu ya NBC atacheza mchezo wa ufunguzi wa ligi yaani Ngao ya Jamii.  Hivyo ni rasmi ufunguzi wa wa ligi kuu mchezo  wa "Ngao ya Jamii msimu huu 2025-2026 ni Yanga na Simba watakutana.

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...