Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KAGERA SUGAR WAPANIA KUISHUSHA SIMBA NAFASI YA NNE

Wakati  mshambuliaji mpya wa Simba Mrundi Amisi Tambwe akirejea uwanjani na kuanza mazoezi, uongozi wa klabu ya Kagera Sugar umetamba kuwa timu yao itaendeleza ubabe dhidi ya 'Wanamsimbazi' kwa kuhakikisha inaibuka na ushindi katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaopigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mechi ya mwisho baina ya timu hizo, Kagera Sugar iliyokuwa ikifundishwa na kocha wa sasa wa Simba, Abdallah Kibadeni, iliwafunga Wekundu wa Msimbazi 1-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba Machi 27, 2013 baada ya timu hizo kutoka sare ya 2-2 jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2012.


Akizungumza na jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Kagera Sugar, Hamis Madachi alisema kikosi chao kinachonolewa na kocha Mganda Jackson Mayanja, kimeandaliwa vizuri kwa ajili ya mchezo huo.

"Hatuna wasiwasi na timu yetu katika mchezo wa  leo kwa sababu tunawaelewa vizuri Simba. Kikosi chetu kilitua Dar es Salaam juzi na jana kinaendelea na mazoezi maeneo ya Tandale kujiweka sawa kabla ya kuwakabili Simba," alisema Madachi na kuongeza:

"Mara nyingi timu za nje ya Dar es Salaam zinapokuja kucheza kwenye Uwanja wa Taifa zinakuwa na hofu lakini sisi hatuna cha kuogopa kwenye Uwanja wa Taifa. Tutaendeleza kipigo kwa Simba leo."

Katika hatua nyingine, mshambuliaji Mrundi Amisi Tambwe wa Simba aliyekosa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara waliyolala 2-1 dhidi ya Azam Jumatatu kutokana na maumivu ya goti, jana alianza mazoezi mepesi kujiandaa kuwakabili Kagera Sugar.

Daktari wa Simba, Yassin Gembe alisema jana kuwa Tambwe alifanya mazoezi mepesi jana asubuhi Bamba Beach, Kigamboni na alitarajiwa kufanya mazoezi jioni pia.

“Baada ya hapo tutaangalia hali yake kama ataweza kucheza kesho (leo) au la. Hatutamlazimisha kucheza kama hajapona sawa sawa, kwa sababu ni hatari kwake na kwa timu pia,” alisema Gembe.

Tambwe, alicheza dakika zote 810 katika mechi tisa za Simba akianza na mchezo wao wa pili msimu huu dhidi ya Oljoro JKT jijini Arusha Agosti 28 akihitimisha katika mchezo wake wa tisa waliotoka suluhu dhidi ya Coastal Union jijini Tanga Oktoba 23.

Simba itarejea kileleni kama itashinda mechi ya leo kwa kuwa itafikisha pointi 23, sawa na vinara Azam na wageni wa ligi hiyo Mbeya City walio katika nafasi ya pili kwa sasa. Tofauti nzuri ya magoli itawabeba Simba.

Yanga, waliopata ushindi wa 3-0 dhidi ya timu ya mkiani mwa msimamo, Mgambo JKT juzi, watashuka kwenye Uwanja wa Taifa kesho kuwakaribisha 'maafande' wa JKT Ruvu katika mechi nyingine ya ligi hiyo.

Keshokutwa kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam) na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).

Raundi ya 12 ya ligi hiyo inayoshirikisha timu 14, itakamilika Jumapili kwa mechi moja, Mbeya City itapokuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.

Novemba 7, Azam itacheza dhidi ya Mbeya City (Azam Complex, Dar es Salaam) wakati Yanga itacheza dhidi ya Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Ngao ya Jamii sasa ni Simba na Yanga

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limebadilisha kanuni za mashindano za Ngao ya Jamii kutoka timu nne na sasa utaratibu utakuwa kama zamani. Bingwa wa Ligi Kuu bara atacheza na mshindi wa kombe la CRDB Cup "CRDB Federation Cup, na endapo kama bingwa wa ligi na CRDB atakuwa ni mmoja basi mshindi wa pili kwenye Ligi Kuu ya NBC atacheza mchezo wa ufunguzi wa ligi yaani Ngao ya Jamii.  Hivyo ni rasmi ufunguzi wa wa ligi kuu mchezo  wa "Ngao ya Jamii msimu huu 2025-2026 ni Yanga na Simba watakutana.

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...