Ruka hadi kwenye maudhui makuu

BRANDTS AHOFIA KAMBI YA PEMBA......

Wakati  mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngasa anaugua malaria na yuko hatarini kuikosa mechi ya Ligi Kuu ya Bara dhidi ya watani wa jadi Simba Jumapili, kocha wa mabingwa hao watetezi Mholanzi Ernie Brandts amesema hajui kwanini wameenda kuweka kambi Pemba.


Ngasa ambaye yuko katika kiwango cha juu akifunga magoli mawili na kutoa pasi mbili za magoli katika mechi tatu alizocheza tangu arejee kutoka kufungiwa mechi sita, alianza kutumia dawa juzi, lakini jana mchana alijilazimisha kufanya mazoezi na wenzake taratibu kwenye Uwanja wa Gombani kabla ya kurejea kupumzika katika hoteli ya Samail walipofikia.

Yanga iliyoondoka Dar es Salaam kwa ndege ya kukodi juzi asubuhi, inajifua katika Uwanja wa Gombani wenye nyasi bandia.

Akizungumzia afya yake, Ngasa alisema hadhani kama itamkosesha kucheza mechi ya Jumapili, kwani ana matumaini ya kupona haraka.

“Nafanya mazoezi mepesi mepesi, naamini hadi siku ya mechi nitakuwa fiti kabisa, kikubwa naomba wanachama na wapenzi wa Yanga waniombee dua nipone ili niisaidie timu Jumapili,” alisema.

Ngasa anasubiriwa kwa hamu Jumapili kuichezea Yanga dhidi ya timu yake ya msimu uliopita Simba aliyojiunga nayo kwa mkopo wa msimu mmoja akitokea Azam.

Ngasa amedhamiria kutoa machungu yake dhidi ya Simba Jumapili baada ya kuitumikia timu hiyo mwaka mzima na kujikuta akiishia kuilipa Sh. milioni 45 kama alivyoamriwa katika adhabu yake iliyotolewa na shirikisho la soka nchini (TFF).

Aidha, Kocha Brandts ametoa kali baada ya kueleza kuwa hajui kwanini kikosi chake kimeweka kambi kisiwani Pemba kujiandaa kwa mchezo unaofuata wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya watani wao wa jadi, Simba.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mazoezi ya Yanga kwenye uwanja wa Gombani, Pemba jana asubuhi, Brandts alisema haelewi kwa nini uongozi umeamua kambi ya timu yake iwekwe Pemba badala ya eneo jingine kujiandaa kwa mchezo huo mgumu dhidi ya vinara wa msimamo wa ligi hiyo.

“Kusema ukweli sijui kwa nini tumekuja Pemba. Ningependelea kuweka kambi yetu sehemu yoyote yenye utulivu na uwanja mzuri kwa ajili ya mazoezi ya timu. Nafikiri viongozi ndiyo wanajua sababu za kutuleta huku (Pemba). Sikuulizwa katika kuchagua eneo la kambi,” alisema Brandts.

“Tumekuja Pemba tukiwa na wachezaji wote 29 walioidhinishwa kuitumikia Yanga msimu huu na wote wanaendelea vizuri na mazoezi kwa ajili ya mchezo wetu wa Jumapili dhidi ya Simba… nafikiri waulize viongozi sababu za kutuleta Pemba katika kipindi hiki,” alisema zaidi Brandts.

Alipoulizwa na mwandishi kuhusu timu yake kuweka kambi Pemba, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh alisema; “hilo ni suala la uongozi. Waulize viongozi maana wao ndiyo waliamua tuje huku (Pemba).”

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alikataa kueleza sababu za timu yao kuweka kambi kisiwani Pemba huku akimtaka mwandishi aulize swali hilo kwa msemaji wa klabu hiyo iliyoanzishwa 1935.

Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto alisema katika mahojiano  jana mchana kuwa waliamua kupeleka kikosi chao Pemba kwa kuwa kuna uwanja mzuri kwa ajili ya mazoezi na kwamba mazingira ya huko yana utulivu ukilinganisha na Dar es Salaam.

“Ni maamuzi tu ya uongozi baada ya kuwasiliana na kocha na kuangalia eneo linalofaa kwa ajili ya kambi ya timu kwa muda huu ambao hatuna mechi kwa wiki nzima,” alisema Kizuguto.

Hiyo ni mara ya pili kwa Yanga kuweka kambi kisiwani Pemba tangu kutua kwa Brandts Septemba mwaka jana kurithi mikoba ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Mbelgiji Tom Saintfiet aliyetimuliwa.

Kabla ya kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa kufunga msimu uliopoita uliopigwa Mei 18 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mabingwa hao mara 23 wa Tanzania Bara (Yanga) waliweka kambi kisiwani Pemba huku ‘Wekundu wa Msimbazi’ wakiweka kambi yao kisiwani Unguja.

Wakati ‘Wanajangwani’ wakirejea tena Pemba kwa ajili ya kambi, Simba wao wameweka kambi yao mjini Bagamoyo, Pwani, mji ambao mara kwa mara Yanga walikuwa wakiutumia kuweka kambi kabla hawajapata mawazo ya kuamua kuhamia Pemba.

Simba na Yanga zimekuwa na desturi ya kuingia ‘mafichoni’ kabla ya kucheza mechi zinazowakutanisha na katika siku za karibuni timu hizo kongwe nchini zimekuwa zikiingia mafichoni kabla ya kucheza dhidi ya Azam FC ambao tayari msimu huu wameifunga Yanga 3-2.

Katika mechi za mwisho, Simba ilishinda 1-0 dhidi ya Prisons kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati Yanga ilishinda 2-1 dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Ngao ya Jamii sasa ni Simba na Yanga

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limebadilisha kanuni za mashindano za Ngao ya Jamii kutoka timu nne na sasa utaratibu utakuwa kama zamani. Bingwa wa Ligi Kuu bara atacheza na mshindi wa kombe la CRDB Cup "CRDB Federation Cup, na endapo kama bingwa wa ligi na CRDB atakuwa ni mmoja basi mshindi wa pili kwenye Ligi Kuu ya NBC atacheza mchezo wa ufunguzi wa ligi yaani Ngao ya Jamii.  Hivyo ni rasmi ufunguzi wa wa ligi kuu mchezo  wa "Ngao ya Jamii msimu huu 2025-2026 ni Yanga na Simba watakutana.

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...