
Akizungumza mara baada ya mchezo wa juzi dhidi ya maafande wa Prisons kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini hapa, Minziro alisema ligi ya msimu huu imeonyesha dalili ya kuwa ngumu zaidi ya msimu uliopita.
“Matokeo ya sare tatu mfululizo tuliyoyapata yanathibitisha hilo. Pamoja na kwamba ligi ndiyo kwanza imeanza, lakini ni wazi kuna dalili zote za ligi kuwa ngumu na tuna kazi kubwa katika kutetea ubingwa wetu,” alisema Minziro.