Ruka hadi kwenye maudhui makuu

YANGA YALIZWA TENA NA AZAM TV

Wakati Kampuni ya Azam Media na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zikisaini rasmi mkataba wa kuonyesha Ligi Tanzania Bara, Klabu ya Yanga imeshangazwa na hatua hiyo ikisema imefanyika kinyume na mapendekezo yake.


Jana, TFF na Azam Media zilisaini mkataba huo wa miaka mitatu utakaogharimu Sh5.6 bilioni, ambapo zitalipwa kwa vipindi vitatu.

Awali, pande hizo mbili ziliingia mkataba wa makubaliano kabla ya jana kusaini mkataba rasmi.

Katika mkataba huo, kila klabu itaweka kibindoni kitita cha Sh100 milioni kutoka Azam Media, ambayo itakuwa inaonyesha ‘Live’ mechi za Ligi Kuu kupitia Azam TV.

Hata hivyo, mkataba wa makubaliano kati ya Azam Media na TFF ulipingwa na klabu ya Yanga, ambayo ilidai ulikuwa na upungufu na kuomba upitiwe upya kabla ya kusainiwa mkataba rasmi.

Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba huo, Makamu wa Pili wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani alisema, fedha zitakazotolewa na Azam Media zitazisaidia klabu kutekeleza mipango ya maendeleo.

“Soka haliwezi kuendeshwa kwa viingilio, mkataba huu utazisaidia klabu kutekeleza mipango ya maendeleo sambamba na kuifanya ligi yetu iwe bora,” alisema Nyamlani.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alisema ameshangazwa na uamuzi wa Azam Media na TFF kusaini mkataba wakati mapendekezo yao hayajafanyiwa kazi.

“Taarifa za kusaini mkataba nimezisikia leo asubuhi, kweli zimenishangaza. Makubaliano yalikuwa, bodi ya Ligi na Azam ziupitie upya kisha mwanasheria wetu auone ndiyo mambo mengine yafuate,” alisema Mwalusako.

Aliongeza: “Siwezi kulizungumzia sana hili, lakini ndiyo yalikuwa makubaliano yetu sasa kama wamesaini bila mapendekezo yetu kufanyiwa kazi ni jambo linaloshtua.”

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC