Ruka hadi kwenye maudhui makuu

YANGA MATAWI YA JUU, YAI[A KIPIGO CHA MBWA MWIZI ASHANTI

Mabingwa watetezi Yanga jana walitumia vizuri ugeni kwenye ligi kuu ya Bara wa Ashanti United iliyokuwa na wachezaji 10 uwanjani kufunga mabao matatu ya mapema katika kila kipindi, yaliyoisaidia kuichabanga 5-1 na kuipa pointi tatu baada ya mchezo mmoja.

Ashanti ilimaliza mchezo huo ikiwa na wachezaji 10 baada ya Emmanuel Kichiba kutolewa uwanjani na muamuzi Israel Nkongo kwa kosa la pili la kadi ya njano katika robo saa ya mwisho.
Kocha wa Yanga, Ernie Brandts alisema alitaraji kiwango cha ushindi ambacho timu yake ilipata kwa sababu aliingiza timu uwanjani akiwa haidharau Ashanti kutokana na kutoifahamu.
Mwalimu wa Ashanti, Hassan Banyai alisema timu yake ilizidiwa kwa sababu ya kuwa na wachezaji wengi wageni kulinganisha na Yanga ambayo ni timu kubwa iliyocheza pamoja kwa muda mrefu.
Nizar Khalfani na Haruna Niyonzima waliifungia Yanga mabao la nne na tano ya mwishoni mwa mchezo, moja katika dakika ya 90, lakini kuchabangwa huko kwa Ashanti kwenye ligi kulijengwa mwanzoni mwa vipindi viwili vya mchezo huo kwenye Uwanja wa Taifa.
Ikionyesha dhahiri mchecheto wa kurudi kwa mara ya kwanza kwenye ligi hiyo ya hadhi ya juu zaidi nchini, Ashanti iliyokuwa na jezi za rangi ya machungwa na bukta nyeusi haikuwa imetulia hivyo kutoa mwanya kwa Yanga kutawala uwanjani katika dakika 15 za kwanza.
Haikushangaza basi kuona Jerry Tegete akiipatia bao la kwanza kutokana na pasi fupi ya Simon Msuva katika dakika ya 10 baada ya mshambuliaji huyo kumzunguka beki wa Ashanti, Tumba Sued, na kuutumbukiza mpira wavuni kirahisi.
Bao la Tegete lilikuja dakika moja tangu Mussa Kanyaga ashindwe kuifungia Ashanti bao la wazi alipompa mpira mikononi Ally Mustafa katika lango la Yanga, baada ya kumtoka Nadir Haroub.
Ashanti ambayo ilielekea haikujifunza kutokana na makosa ya dakika za mwanzoni za kipindi cha kwanza, ilijikuta ikifungwa mabao mawili ya haraka ndani ya dakika 12 za kwanza za kipindi cha pili pia.
Mpishi wa bao la kwanza Msuva aliifungia Yanga goli la pili dakika mbili tangu kuanza kwa ngwe ya pili, baada ya kupiga shuti la mbali lililokwenda moja kwa moja wavuni.
Ilimchukua Tegete dakika 10 zaidi kuifungia Yanga bao ambalo lilimaliza ushindani wa mechi hiyo na kuihakikishia Yanga mwanzo mzuri wa msimu mpya, aliposhirikiana tena na Msuva kutumbukiza mpira wavuni.
Khalfani aliifungia Yanga bao la tano katika dakika ya mwisho ya mchezo kutokana na pasi ya Domayo wakati Niyonzima aliifungia bao la nne zikiwa zimebaki dakika 17 mpira kumalizika.
Bao la kupoza machungu kwa Ashanti lilifungwa na Shaban Juma aliyeingia kutoka benchi, dakika moja kabla ya goli la Khalfani.
Timu zilikuwa:
YANGA: Ally Mustafa, Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub, Mbuyu Twite, Athumani Iddi (Frank Damayo dk.18), Simon Msuva, Salum Telela, Didier Kavumbagu, Jerry Tegete (Nizar Khalfani dk.81), Haruna Niyonzima.
ASHANTI: Ibrahim Abdallah, Khan Usimba, Emmanuel Kichiba, Ramadhani Malima, Tumba Sued, Emmanuel Memba, Fakihi Hakika, Mussa Nampaka (Laurent Mugia dk.61), Hussein Sued, Musa Kanyaga, Joseph Mahundi (Hussein Mkongo dk.84).

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC