SAMUEL ETO'O AKARIBIA KUTUA CHELSEA, KUMWAGA WINO NDANI YA MASAA 48


KLABU ya Chelsea iko katika hatua za mwishoni za kukamilisha usajili wa Samuel Eto'o kutoka Anzhi Makhachkala na dili hilo linaweza kukamilika ndani ya saa 48.


Tayari wamekwishamsajili Willian kutoka Anzhi ambaye anasubiri kibali cha kufanya kazi leo na usajili wa Eto'o utakuwa sehemu ya Pauni Milioni 32 zilizotengwa.

Mkataba wa mshambuliaji huyo wa Cameroon utakuwa mfupi tu wa mwaka mmoja.

Eto'o alianzia soka yake Ulaya katika klabu ya Real Madrid, lakini alicheza mechi tatu tu na akapelekwa kwa mkopo katika miaka yake minne na klabu hiyo ya Jiji la Hispania.

Alitengeneza jina alipokuwa akichezea Mallorca kabla ya kusajiliwa na Barcelona. Aliiwezesha kushinda Ligi ya Mabingwa, akifunga dhidi ya Arsenal katika Fainali mwaka 2006.

Baadaye akaenda kuungana na Jose Mourinho Inter Milan, na hiyo inaweza kuwa sababu moja ya kuchaua kutua Chelsea. Kocha huyo Mreno anaweza kuwa na imani naye zaidi kuliko washambuliaji wake wa sasa, Fernando Torres, Romelu Lukaku au Demba Ba.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI